RUGE MUTAHABA |
NAIBU WAZIRI HABARI NA MICHEZO AMOS MAKALLA |
LADY JAYDEE |
Na Mwandishi Wetu
IKIWA ni siku moja tu tangu Naibu Waziri wa Habari Michezo
Vijana na Utamaduni Amos Makala kutangaza hadharani kulivalia njuga
suala la mzozo kati ya Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media Group
Ruge Mutahaba na msanii nyota wa kike wa Bongo Fleva Judith ‘Wambura Lady Jaydee’ Ruge ametoa ya moyoni.
Mwandishi wa blog hii ambaye alimpigia simu Ruge na kumuuliza ana lipi la kusema baada
ya Makala kutamka kwamba atawaita wawili hao na kuzungumza nao sambamba
na kuleta suluhu.
“Mimi kana nilivyosema katika tamko langu wiki iliyopita kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize pande zote mbili hasa
mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady
Jaydee amekuwa akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa
kumuelewa”
Na
siyo Waziri Makalla tu pia ikiwezekana hata kama kuna watu wengine
wanataka kujitokeza ili kutuweka katika kiti moto watuulize maswali na
kila mmoja wetu aote majibu mbele ya hao watu mimi niko radhi kufanya
hivyo” anasema Ruge.
Wakati huohuo Ruge ameongeza kwamba tayari
ameshatoa fuara taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungua
jalada la malalamiko ya kutukanwa na Lady Jaydee na taarifa hiyo
amepelekewa msanii huyo akiitwa katika vyombo vya sheria.
Lakini
ninaweza kusema jambo hili linaweza kuzungumzika nje ya vyombo vya
sheria kwani sisi tunaliona ni jambo dogo na la mzaha lakini lina athari
kubwa katika jamii inayotuzunguka anasema Ruge.
Mwanzoni mwa mwezi huu Lady Jaydee aliamua kuibuka na kuituhumu Clouds Media Group kwa
kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter nab log yake kwamba
wana muhujumu kimuziki , kuzuia matangazo ya mgahawa wake wa Nyumbani
Lounge na kipaji chake kwa ujumba tuhuma ambazo Ruge na Clouds wanazikanusha vikali.
Mwandishi
wa habari hii alijaribu kumtafuta Lady Jaydee azungumzie kuhusu kauli
ya Waziri kwa kupitia simu ya mumewake Gadner Habash simu iliita bila
kupokelewa.
No comments:
Post a Comment