Sunday, June 16, 2013

KUFUATIA MLIPUKO WA JANA,TUME YA UCHAGUZI IMEAHIRISHA KUFANYIKA KWA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATIKA KATA TANO ZA JIJI LA ARUSHA

MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JAJI MSTAAFU DAMIAN LUBUVA
Tume ya taifa ya uchaguzi imeahirisha kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata tano za jiji la Arusha uliopangwa kufanyika hii leo,kufuatia tukio la mlipuko uliotokea jana huko Mkoani Arusha katika mkutano wa kuhitimisha kampeni kwa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,na kusababisha watu watatu kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya na mlipuko huo.
Akizungumza na mwandishi wa blog hii kwa njia ya simu kutoka Zanzibar,mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema uchaguzi huo utafanyika June 30 mwaka huu na kwamba hali hiyo itawapa nafasi vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha zaidi ulinzi siku ya uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...