Friday, June 14, 2013

TARATIBU ZA MAZISHI YA LANGA

marehemu Langa


akihojiwa katiaka studio za East africa Radio wakati anaitambulisha track yake mpya
Ratiba ya mazishi ya ndugu yetu Langa Kileo itakuwa kama ifuatavyo, msiba upo nyumbani kwa wazazi wa Langa maeneo ya Mikocheni nyuma ya Hospitali ya AAR zamani kulikuwa na ofisi za Benchmark Production. Mwili wa marehemu utaagwa siku ya Jumatatu majira ya saa 7 mchana na baada ya hapo mwili utaelekea makaburi ya Kinondoni kwa mazishi majira ya saa kumi alasiri.
Langa amefariki dunia jana katika hospitali ya taifa muhimbili baada ya kuugua malaria kali na alifariki dunia saa 11 jioni katika hospitali hiyo akitokea katika hospitali ya Dr Mvungi iliyopo kinondoni jijini Dar es Salaam.
Langa alianza kutambulika katika medani ya muziki wa hip hop mwaka 2004 akiibuka katika kundi la WAKILISHA lililopatikana katika mashindano ya Coca cola pop stars likiundwa na wasanii wengine Witness pamoja na Shaa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...