Wednesday, July 31, 2013

TCRA YAZINDUA KAMPENI MPYA YA UHAMASISHAJI WA MATUMIZI MAZURI YA MAWASILIANO

MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA PROF JOHN NKOMA AKIZUNGUMZA NA WADAU WA HABARI

MENEJA WA MAWASILIANO WA TCRA INNOCENT MUNGI AKIFAFANUA JAMBO



MRISHO MPOTO AKIFURAHIA JAMBO

MDAU NA MMILIKI WA BLOG YA FULL SHANGWE AKIWASHUKURU TCRA KWA KUTAMBUA BLOGS KAMA VYOMBO VYA HABARI KWA NIABA YA BLOGGERS WENGINE



MAPAPARAZI KAZINI

WANAHABARI WAKISIKILIZA KWA MAKINI-PICHA ZOTE NA MTAA KWA MTAA BLOG

WASHINDI WATANO WA TIGO “MILIKI BIASHARA YAKO” WAKABIDHIWA BAJAJI ZAO KWA FURAHA NA BASHASHA LEO

 Mshindi wa promosheni ya Tigo “Miliki Biashara Yako” Bw. Nicolaus Sanga (43) akijaribu Bajaji yake mpya yenye thamani ya Tsh 6,700,000 aliyokabidhiwa kutoka kwa Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga anayeshuhudia.
Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga (katikati) akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mmoja wa washindi wa promosheni “Miliki Biashara Yako” Bi. Isabella Msemo (24) katika hafla iliyofanyika Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Bidhaa wa Tigo Bw. Husni Seif. 
 Mshindi wa Tigo “Miliki Biashara Yako” Bi.  Evelyn Massawe (22) mkazi wa Dar es Salaam ambaye ni mwanafunzi wa chuo MAKUMIRA akipokea ufunguo wa Bajaji yake mpya yenye thamani ya Tsh 6,700,000 kutoka Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga katika hafla iliyofanyika Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam.
 Mshindi wa Tigo “Miliki Biashara Yako” Bi. Evelyn Massawe (22) kwa furaha akijaribu Bajaji yake mpya yenye thamani ya Tsh 6,700,000 aliyokabidhiwa na Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga katika hafla iliyofanyika Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam.
  Mshindi wa Tigo “Miliki Biashara Yako” Bw. Khalid Gomani (27) akikagua Bajaji yake mpya mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga (kushoto). Bajaji hizo zina warranti ya miezi 7.
 Washindi wa Tigo “Miliki Biashara Yako” wakipongezana mara baada ya kukabidhiwa Bajaji zao rasmi na Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga (katikati). Tigo tayari imelipia leseni ya barabarani (road license) na bima kwa ajili ya Bajaji hizo.
 Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga katika mahojiano na Waandishi wa Habari. Kwanza aliwapongeza washindi wote 7 wa droo hii ya pili, pia alikumbushia kwamba kila mteja wa Tigo anao uwezo wa kujishindia Bajaji moja kila siku kwa muda wa siku 60 kwa kuongeza vocha ya Tsh 1,000 tu kwa siku. Ili kuhakikisha kuwa wateja wengi wanafurahia promosheni hii, mteja hahitaji kuweka vocha ya Tsh 1000 kwa mkupuo mmoja ili kushiriki, anaweza kuongeza salio kidogo kidogo hadi kufikisha kiasi cha Tsh 1000 kwa siku na kuweza kuingia kwenye droo. Bajaji 50 zimebaki kushindaniwa.
Washindi wa Tigo “Miliki Biashara Yako” ibuka na Bajaji katika picha ya pamoja na Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga (watatu kushoto).

ZIARA YA OMMY DIMPLES BURUNDI ANGALIA VIDEO AKIJINADI

ZIARA YA MH AGREY MWANRY WILAYANI LUSHOTO

JENGO LA OFISI YA MKURUGENZI WA WILAYA YA LUSHOTO LILILOKAGULIWA NA NAIBU WAZIRI MH AGREY MWANRY

MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO MH ALHAJ MAJID MWANGA NA NAIBU WAZIRI MH AGREY MWANRY ALIYECHUCHUMAA AKIKAGUA CULVERT KATIKA BARA BARA YA BOMANI MAGUZONI WILAYANI LUSHOTO

Tuesday, July 30, 2013

JELA MIAKA 30 KWA KUMBAKA NA KUMZALISHA BINTI YAKE WA KUMZAA


Yusufu Amani (39) aliyembaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe Afungwa miaka 30
Hapa akijifunika sipigwe picha baada ya hukumu
Kulia ni mtoto aliyebakwa na baba yake kisha kuzalishwa akiwa na mtoto wake wakitoka mahakamani kulia ni mama mzazi wa binti aliyebakwa na kuzalishwa


MAHAKAMA ya wilaya ya Mbeya imemhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi wa Isanga Mkoani hapa baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti na kumzalisha binti yake wa kumzaa akiwa na miaka 15( jina linahifadhiwa).



Mwendesha mashitaka wa serikali  Archiles Mulisa  aliiambia mahakamani hiyo Mbele ya Hakimu Gilbert Ndeuruo kuwa Mshtakiwa huyo ni Yusufu Amani (39) anayedaiwa kumbaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe.



Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 154 (1)a na 155 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho  mwaka 2002, pamoja na kifungu cha 158(a) cha makosa ya kuzini.


akisoma Hukumu hiyo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mtuhumiwa alianza kujihusisha kimapenzi na mwanaye Mwaka 2008 baada ya kutengana na mkewe ambapo Mtuhumiwa aliachiwa watoto wote.
Aliongeza kuwa wakati huo binti huyo alikuwa na umri wa miaka 12 na alikuwa akisoma shule ya msingi darasa la Tano jambo ambalo wamedumu nalo kwa Miaka mine hadi ilipogundulika kuwa binti alikuwa mjamzito Mei, 2012.
Alisema mbinu aliyokuwa akiitumia ni kumtishia binti asitoe taarifa kwa mtu yoyote na kwamba baada ya kugundulika kuwa na ujauzito alimwambia amsingizie kijana yoyote mtaani kwao.
Hakimu Ndeuruo alisema Mahakama ilimtia hatiani Mtuhumiwa kutokana na ushahidi wa Mhanga wa tukio hilo ambaye ni binti pamoja na ushahidi wa kitaalamu kutoka kwa Mkemia mkuu wa Serikali.
Alisema ushahidi wa Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kupima Vinasaba kutoka Mtuhumiwa, Mhanga na Mtoto aliyezaliwa ulidai kuwa  Mshtakiwa ndiye baba halali wa Mtoto kutokana na Maeneo 15 ya vipimo vya Vinasaba kati ya Baba na Mtoto aliyezaliwa kufungana kwa asilimia 99.9.
Aidha kabla ya kutoa hukumu Hakimu alimpa nafasi mtuhumiwa kujitetea ili apunguziwe adhabu au asiweze kuhukumiwa kabisa lakini hali ikawa tofauti baada ya Mtuhumiwa kujibu kuwa hana la kujitetea vyovyote itakavyokuwa anachotaka ni nakala ya hukumu.
Kutokana na kushindwa kujitetea Hakimu Ndeuruo alimhukumu kwenda jela miaka 30 na kwamba ana haki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu endapo hakuridhika na hukumu hiyo.
Awali katika ushahidi wake Mahakamani hapo Mtuhumiwa huyo alidai kuwa hakutenda kosa hilo bali alitengenezewa na Mkewe ambaye aliapa kumkomesha baada ya kukosana na kumpata mume mwingine jambo ambalo lilipingwa vikali na hakimu na kudai kuwa “ mfa maji haachi kutapatapa”

Na Mbeya yetu

Monday, July 29, 2013

DEREVA BODA BODA MJINI IRINGA ATEKWA ACHOMWA KISU


Madereva  boda boda  wakimfariji mwenzao
Madereva  boda  boda  wakiwa  eneo la Embakas Gereji ambako  watekaji  waliamua  kutelekeza  pikipiki  waliyoiteka
Mwanzo  wa msako  wa kusaka  watekaji wa madereva  boda boda mjini Iringa ukianza
Hii ndio  pikipiki iliyotekwa na kutelekezwa hapa eneo la Ilala mjini Iringa
Boda  boda  iliyotekwa ikiwa imepatikana
Askari  polisi  wakiwa wamepakia boda  boda  hiyo  iliyokuwa imetekwa
Hapa madereva  boda  boda  wakiwa nje ya Hospital ya mkoa  wa Iringa kumtazama mwenzao
Wimbi  la  watu  wanaoteka  boda  boda  limeendelea  kutikisa katika maeneo mbali mbali ya mji  wa Iringa hali  inayotishia amani  ya  madereva  boda boda mjini hapa.

Kutokana na  kuongezeka kwa matukio ya  utekaji ,madereva  wa boda  boda  wameamua  kuanzisha msako mkali katika maeneo mbali mbali ya mji ili  kupambana na watekaji hao kwa  kutumia dhana ya polisi jamii na ulinzi  shirikishi.

Hali  hiyo imekuja baada ya madereva  zaidi ya wawili  kutekwa na kupokonywa  pikipiki  zao ndani ya  wiki moja huku mmoja akinusurika  kuuwawa kwa kuchomwa  kisu .habari/picha na francis godwin

PERSONALLY,PERSONALLY DAAAAH PSQUARE ENJOY

RAIS KIKWETE ALIPOMTEMBELEA HOSPITALI MMILIKI WA HOME SHOPPING CENTRE AFRICA KUSINI

RAIS JAKAYA KIKWETE ALIVYOMTEMBELEA MMILIKI WA MADUKA YA HOME SHOPPING CENTRE SAID MOHAMMED SAAD AFRIKA KUSINI BAADA YA KUMWAGIWA TINDIKALI HIVI KARIBUNI

Saturday, July 27, 2013

ZIARA YA RAIS KIKWETE WILAYANI MULEBA

Wananchi wa Muleba wakimshangilia Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili wilayani humo akiwa katika ziara yake ya siku sita Mkoani Kagera
Rais Kikwete akivikwa skafu na skauti baada ya kuwasili Muleba
Vikundi vya ngoma vikitumbuiza wageni
Rais Kikwete akisalimiana na mama wa Profesa Anna Tibaijuka
Waziri wa Ardhi Profesa Anna Tibaijuka akishiriki katika ngoma ya utamaduni wakati wa mapokezi ya Rais Kikwete wilayani Muleba
Rais Kikwete akiongea na viongozi wa wilaya ya Muleba baada ya kupokea taarifa ya maendeleo, akiwa na mawaziri watano anaoongozana nao katika ziara hiyo
Mbunge wa Muleba akitoa  maoni na kero za jimbo lake
Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe akiwahakikishia viongozi wa Muleba juu ya mipango ya serikali kuleta meli za abiria mpya mbili katika ziwa Victoria
Rais Kikwete akipata maelezo ya mpango kabambe wa maji wilaya ya Muleba
Rais Kikwete akizindua mradi mkubwa wa maji wilayani Muleba
Rais Kikwete akikata utepe kuzindua mradi wa maji
Rais Kikwete akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wananchi wa Muleba baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji kwa wilaya hiyo
Mwananchi mwingine akitwishwa maji
Ngoma ya utamaduni ikimlaki Rais Kikwete alipowasili katika mkutano wa hadhara
Rais Kikwete akisalimia wananchi
Rais Kikwete akiangalia mazao yatokanayo na uzalishaji mbegu ya kampuni ya Itente ya Muleba
Rais Kikwete akipozi na wafanyakazi wa kampuni ya uzalishaji mbegu ya Itente
Rais Kikwete akifurahia ngoma
Umati wa wananchi Muleba ukimsikiliza Rais Kikwete
Rais Kikwete akiongea na wananchi wa Muleba
Rais Kikwete akihutubia wana Muleba
Sehemu ya umati mkutanoni
Rais Kikwete akiendelea kungea na wananchi
Umati  katika mkutano wa hadhara
Umati katika mkutano wa hadhara
Rais Kikwete akijiunga na waumini wa Muleba kusali swala ya Magharibi kabla ya kufuturu
Dua ikisomwa baada ya futari aliyoandaa Rais Kikwete kwa wananchi wa Muleba
Dua ikiombwa baada ya futari
Dua
Wananchi wa Muleba katika futari aliyoandaa Rais Kikwete wilayani Muleba
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...