Monday, July 29, 2013

DEREVA BODA BODA MJINI IRINGA ATEKWA ACHOMWA KISU


Madereva  boda boda  wakimfariji mwenzao
Madereva  boda  boda  wakiwa  eneo la Embakas Gereji ambako  watekaji  waliamua  kutelekeza  pikipiki  waliyoiteka
Mwanzo  wa msako  wa kusaka  watekaji wa madereva  boda boda mjini Iringa ukianza
Hii ndio  pikipiki iliyotekwa na kutelekezwa hapa eneo la Ilala mjini Iringa
Boda  boda  iliyotekwa ikiwa imepatikana
Askari  polisi  wakiwa wamepakia boda  boda  hiyo  iliyokuwa imetekwa
Hapa madereva  boda  boda  wakiwa nje ya Hospital ya mkoa  wa Iringa kumtazama mwenzao
Wimbi  la  watu  wanaoteka  boda  boda  limeendelea  kutikisa katika maeneo mbali mbali ya mji  wa Iringa hali  inayotishia amani  ya  madereva  boda boda mjini hapa.

Kutokana na  kuongezeka kwa matukio ya  utekaji ,madereva  wa boda  boda  wameamua  kuanzisha msako mkali katika maeneo mbali mbali ya mji ili  kupambana na watekaji hao kwa  kutumia dhana ya polisi jamii na ulinzi  shirikishi.

Hali  hiyo imekuja baada ya madereva  zaidi ya wawili  kutekwa na kupokonywa  pikipiki  zao ndani ya  wiki moja huku mmoja akinusurika  kuuwawa kwa kuchomwa  kisu .habari/picha na francis godwin

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...