Friday, July 12, 2013

DEREVA WA DALADALA ASUSIWA MAITI BAADA YA KUZAA NA MWANAFUNZI

 Mwenyekiti wa Mtaa wa Ihanga Kata ya Ilomba Emanuel Mwasibata akiwa amesimamia kikao cha usuruhishi
 Dereva wa daladala Aswile Mwalukoba aliyeshika fimbo baada ya kurejea nyumbani na kuhudhuria kikao cha usuruishi  ambapo alikili kuzaa  na mwanafunzi huyo na kukubali kuzika .
 Daladala iliyobeba mwili wa Marehemu kutoka Uyole.
 Wakazi wa Uyole wakiwa wameshikwa na butwaa baada yakumkosa mwenyeji wao
 Mwili wa mtoto ukiwa umefunkwa na kitenge na kutelekezwa kwenye kiti
 Kulia ni Carolina Kyando akiwa na dada yake baada ya kuleta mwili wa mtoto nyumbani kwa Mwalukoba eneo la Mama John jijini Mbeya
Majirani pande zote mbili wakingojea kujua hatma ya mazungumzo yanayo endelea baada ya Mwalukoba kurejea


******************
Ezekiel Kamanga
Vitendo vya ukatili dhidi ya  watoto na wanawake  jijini mbeya vimeendelea chukua sura mpya  baada ya dereva wa daladala jijini humo kumzalisha mwanafunzi Masomo ya jioni kituo cha Juhudi kilichopo  Ilomba.
.
 Tukio hilo limetokea hivi karibuni  eneo la mama John Mtaa wa Ihanga Kata ya Ilomba ambapo dereva wa daladala aliyefahamika kwa jina la Aswile Mwalukoba (45 ) kutelekezewa wa miezi saba ambaye alikwisha fariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti Mtaa huo Ndugu Emanuel Mwasibata amesema kuwa mgogoro huo umetokana  na dereva huyo kugoma kuuzika mwili huo kwakile alicho dai kuwa hivi sasa haishi na binti huyo kwa muda mrefu sasa.
Kwa upande wake binti huyo aliyefahamika kwa jina la Calorina Kyando amedai kuwa kitendo cha yeye kuuchukua mwili wa mtoto huyo hadi kwa baba yake unatokana   kutelekezwa na bwana huyo kisha kupigwa marakwa mara na kusababishiwa ulemavu wa sikio la kushoto baada ya kung’atwa na mwanaume huyo.
Mwanamke huyo amefafanua kuwa mara baada ya mtoto huyo kufariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospital ya Igawilo jijini humo aliamua kumpigia simu mzazi mwenzie kwa lengo la kumpa taarifa za msiba huo.
Amesema mara baada ya kutoa taarifa hiyo mwanaume huyo alikubali na kumueleza mwanamke huyo kuwa yuko tayari kwa ajili ya mazikoya mtoto huyo ambapo anafanya taratibu za kuwasiliana na ndugu zake walioko Tukuyu Wilayani Rungwe.
Amesema katika siku iliyofuata mwanaume huyo hakupatikana kwa simu ya kiganjani na wala hakuwepo nyumbani kwake anapo ishi eneo la Mama John hali iliyo plelekea baadhi ya majirani na mwanamke huyo kutoka Uyole kusaidiana na kuutoa mwili huo Hospitalini hapo kwa lengo la kufanya taratibu nyingine .
Aidha majirani hao waliamua kuchukua mwili huo hadi nyumbani kwa Mwalukoba ambapo waliuweka kwenye kiti ndani ya nyumba yake huku wakiendelea kumsubiri mwalukoba arudi aliko  ambapo baadaye alirudi nyumbani hapo akisindikiazwa na Mdogo wake aliyefahamika kwa jina Gabriel Mwalukoba hadi nyumbani hapo.
Kitendo hicho cha kurejea kwa mwanaume huyo kilifanya mwenyekiti wa mtaa huo Ndugu Emanuel Mwasibata kuhoji juu ya  kutoweka kwa nyumbani kwakwe kwa muda wa siku mbili huku kukiwa hakuna mawasiliano yoyote.
 Baada ya kikao cha muda mrefu kati ya pande zote mbili mwanaume huyo alikubali kuupokea mwili huo na hivyo kuanza kufanya taratibu za mazishi ambapo mazishi hayo yalifanyika katika makaburi ya Iyela mida saa 12 jioni na kuhudhuriwa na familia zote mbili pamoja na majirani wengine kutoka Uyole na Mama John.
NA MBEYA YETU 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...