Na Muhidin
Amri--Mbinga,
BAADHI ya
askari polisi wa kituo kikuu Mbinga
mjini,wamemtuhumu mkuu wa polisi wa wilaya hiyo(OCD)Jastine Joseph kuwa ni mtu
anayetumia madaraka yake vibaya kwa kuendesha manyanyaso dhidi ya askari wa
vyeo vya chini na kumuomba Mkuu wa jeshi ilo Said Mwema kumuondoa haraka kabla
ya hali haijawa mbaya zaidi.
Wakizungumza
na Gazeti ili kwa masharti ya kutotajwa majina yao,askari hao wamelalamika
kuwa Ocd wao amekuwa akitoa lugha za dharau na hata zisizopendeza kwao hali
inayowavunja moyo wa kazi askari wengine katika wilaya hiyo.
Walisema,iwapo
jeshi litashindwa kumuhamisha Jastine kunaweza kutokea maafa makubwa kwani
hawatoweza kuvumilia vitendo vinavyofanywa na afisa huyo hasa ukizingatia kuwa
na wao ni watu wakubwa tena wenye familia kama yeye hivyo kitendo cha
kuwatolea lugha za kiuni ni sawa na kuwadhalilisha.
Aidha
wameshauri hata maafisa wengine katika wilaya hiyo wanatakiwa kuondoka kwani
wameshaaka Mbinga kwa muda mrefu hivyo ni vema kupelekwa katika maeneo mengine
ya nchi ili wakapate changamoto mpya za utendaji wa kazi, na kuendelea kuwepo
katika wilaya hiyo ni tatizo kubwa kwani wameshafahamika na watu wengine hali
inayowafanya kushindwa kuchukua maamuzi sahihi.
Wamesema ocd
wao ni mtu hasiyetaka ushauri kutoka kwa mwingine hata kwa maafisa wenzake
jambo linalomfanya kutengwa na kujikuta na yuko pekee yake au na wale askari wa
kabila lake tu jambo lililowafanya askari kuwepo katika makundi hasa baada ya
kufika Jastine kitu ambacho siku za nyuma hakikuwepo na askari wote walikuwa
ndugu moja wakiishi na kusaidiana tofauti na sasa.
“huyu mkuu
wetu ni tatizo kubwa,sijui hata mtu aliyempendekeza kuwa ocd ametumia kigezo
gani,hafai kabisa yeye kazi yake ni
majungu tu na sio vinginevyo”alisema mmoja wa askari hao.
Kwa upande
wake Jastine alikanusha tuhuma hizo na kuziita kuwa ni unafiki unaofanywa na
askari wachache waliozoea kula rushwa kila mara hasa kwa waendesha pikipiki
jambo ambalo yeye hataki kusikia katika uongozi wake.
“hizo tuhuma
sio za kweli,zinafanywa na baadhi ya askari wngu hasa wale wala
rushwa,nimeshaelekeza wakikamata pikipiki waje na faini hapa au mmiliki wake
sio kuleta pikipiki hatuna eneo la kupaki kwani hizi tulizonazo ni nyingi na
hatuna sehemu ya kuzipeleka”alisema.
Naye Kamanda
wa polisi mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki alikiri kuwepo kwa malalamiko ya askari wa vyeo vya chini dhidi ya Ocd wao
na kuhaidia kuwa atashughulikia tuhuma hizo ili kupata ukweli wa jambo ilo.
“sisi
hatufanyi mambo kwa kukurupuka tu lazima tufanye uchunguzi ili tujiridhishe,unajua ukishakuwa kiongozi
unatakiwa kuwa makini hasa katika maamuzi ili usifanye mambo kwa kumuonea mtu lazima utende haki
kila wakati”alisema Rpc
No comments:
Post a Comment