Picha kwa hisani ya mtandao
Na Steven Augustino wa demashonews, Tunduru
MKAZI wa Kijiji cha Muhuwesi Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma Mfaume
Mustafa (29) amefariki dunia katika ajali mabaya iliyo sababishwa na
kuumwa na joka kubwa ambalo linadaiwa kuwavamia wakati wakichimba
madini.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa katika tukio hilo marehemu na
wenzake walikubwa na mkasa huo wakati wakichimba madini ya vito
katika eneo laa Namasimba lililopo katika Mto Muhuwesi Wilayani humo.
Taarifa hizo ziliendelea kufafanua kuwa wakiwa wanaendelea na shughuli
zao katika eneo hilo Joka hilo liliibuka kutoka katika mapango ya mawe
na kuanza kuwafukuza na kufanikiwa kumuuma zaidi ya mara tatu na
hatimaye kumwacha akiwa katika maumivu makali.
Walisema baada ya tukio hilo wenzake walipiga Kelele za kuomba msaada
ambapo wasamalia wema walijitokeza na kumbeba majeruhi huyo na
kumkimbiza katika Zahanati ya Kijiji cha Muhuwesi ambapo alifariki
wakati akipatiwa matibabu.
Akizungumzia tukio hilo Diwani wa kata hiyo Nurdin Mnolela pamoja na
kudhibitisha kuwepo kwa tukio la kifo hicho alisema kuwa baada ya
maafisa tabibu kudhibitisha tukio la kifo wanafamilia walichukua mwili
wa ndugu yao na kuuhamishia nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya
maziko.
Alisema wakiwa katika harakati hizo alitekea mtu aliye jiita mganga wa
jadi ambaye aliwarubuni kwa kuwaeleza kuwa anao uwezo wa kumtibu na
kumfufua ndugu yao hali ambayo iliwafanya kuamini na kuanza kutumia
fedha nyingi kwa ajili ya matibabu hayo ambayo hayakuzaa matunda hadi
walipo kubali kumzika baada ya kuona mwili wake umeanza kuharibika
siku ya tatu na sangoma huyo kuingia mitini.
Mwisho
No comments:
Post a Comment