Tuesday, October 1, 2013

MKUU WA WILAYA YA BAHI BETTY MKWASSA ATOA ZAWADI YA KUMBUKUMBU KWA UONGOZI ITV/RADIO ONE IKIWA NI SHUKRANI KWA KUFANYA KAZI KATIKA KAMPUNI HIYO HADI ALIPOONEKANA NA KUTEULIWA KUWA MKUU WA WILAYA


MKUU WA WILAYA YA BAHI BI BETTY MKWASSA AKIIFUNGUA ZAWADI

ZAWADI MEZANI TAYARI KUFUNGULIWA,PICHANI NI MKUU WA WILAYA YA BAHI BI BETTY MKWASSA NA BINTI YAKE

FUNGUA TUONE YALIYOMO,...MKUU WA WILAYA YA BAHI BI BETTY MKWASA AKIIFUNGUA ZAWADI HIYO HUKU MKURUGENZI MTENDANI WA ITV/RADIO ONE JOYCE MHAVILLE AKIMSAIDIA

YVONNE MSEMEMBO AKIMPONGEZA MKUU WA WILAYA YA BAHI BI BETTY MKWASA


MKURUGENZI MTENDAJI WA ITV/RADIO ONE JOYCE MHAVILLE AKIHOJIWA

MKUU WA WILAYA YA BAHI BETTY MKWASA AKISIKILIZA MAHOJIANO KWA MAKINI

MKURUGENZI MTENDAJI WA ITV/RADIO ONE JOYCE MHAVILLE AKICHEKA KWA FURAHA BAADA YA KUKABIDHIWA ZAWADI HIYO YA KUMBUKUMBU

MKUU WA WILAYA YA BAHI MH BETTY MKWASA AKIWA NA BINTI YAKE


MKUU WA WILAYA YA BAHI BETTY MKWASA AKIMKABIDHI ZAWADI YA SAA YENYE PICHA ZA VIONGOZI WA ITV/RADIO ONE MKUREGENZI MTENDAJI ITV/RADIO ONE JOYCE MHAVILLE
Mkuu wa wilaya ya Bahi Bi Betty Mkwassa ametembelea ofisi yake ya zamani ITV/RADIO ONE na kutoa zawadi kwa uongozi ikiwa ni ishara ya shukrani kwa kufanya nae kazi muda mrefu hadi alipoteuliwa kuwa mkuu wa wilaya.

Mkuu huyo wa wilaya alimkabidhi Mkurugenzi mtendaji wa ITV/RADIO ONE, JOYCE MHAVILLE saa yenye picha za baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo.

Akikabidhi saa hiyo mkuu huyo wa wilaya amesema amekaa na kutafakari muda mrefu ni zawadi gani ambayo angeileta ili kuonyesha shukrani zake kwa ITV/RADIO ONE,ndipo alipopata jibu la zawadi na akaona ni vema akatafuta zawadi ambayo itakuwa ni kumbukumbu ya muda mrefu na hata watakaokuja baadae watatambua katika kampuni hii kulikuwa na viongozi hawa ambao picha zao zipo kwenye saa hiyo.

Nae Mkurugenzi mtendaji wa ITV/RADIO ONE, JOYCE MHAVILLE amemshukuru BETTY MKWASSA kwa moyo wake huo kwani ameonyesha kujali na kuthamini kule alikotoka kwani ni watu wachache sana wanaoweza kufanya kama alivyofanya Betty na ameshukuru kwa zawadi hiyo kwani ni ya aina yake na itadumu kwa muda mrefu.

Kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya Betty Mkwassa alikuwa muandishi na mtangazaji wa habari mwandamizi wa ITV/RADIO ONE na alishawahi kuiletea heshma ITV/RADIO ONE na tasnia nzima ya habari hapa nchini baada ya kushinda tuzo ya CNN kupitia kipindi cha UKIMWI NI HUU.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...