Monday, December 23, 2013

INASIKITISHA SANA: KAKA AKIRI KUMCHINJA MDOGO WAKE BAADA YA BABA YAKE KUMUANDIKISHA MALI ZOTE MTOTO WA MKE MDOGO


Mtoto Kalebu Simwelu(6) enzi za uhai wake, mtoto huyu alichinjwa na kaka yake kwa madai kuwa baba yake alimrithisha mali zote.
Mwili wa marehemu Kalebu ukiingizwa katika makazi yake ya milele katika makaburi ya Nakonde nchini Zambia.
Ibada ya mazishi ikiendelea katika makaburi ya Nakonde nchini Zambia
Umati wa waombolezaji uliohudhuria maziko ya mtoto Kalebu ambaye aliuawa kwa kuchinjwa na kaka yake aliyedai kuwa baba yao amemuandikisha mali zote.
Jamaa na ndugu wakiendelea na mazishi katika makaburi ya Nakonde nchini Zambia ambako mtoto Kalebu alizikwa.
KATIKA hali isiyo ya kawaida mmoja wa watoto wa Diwani wa Kata ya Nkangamo Weston Simwelu(55) ambaye watoto wake waliuawa kwa kuchinjwa na kunyongwa,Enock Simwelu(23) amekiri kufanya mauaji hayo kwa madai kuwa yametokana na baba yao kumrithisha mali zote marehemu mdogo wao.
Mauaji hayo yalitokea Disemba 19 eneo la TAZARA katika mji mdogo wa Tunduma ambapo wauaji walivamia nyumbani kwa Diwani huyo na kufanya mauaji ambapo walimchinja kwa kisu mtoto Kalebu Simwelu(6) na mfanyakazi wa ndani Sista Nyirenge(17) na miili yao kuficha sebuleni nyuma ya kochi.
Imeelezwa kuwa Enock pamoja na nduguye wa mama mmoja Gabriel walishirikiana kwa pamoja kufanya mauaji hayo kwa madai ya baba yao kufanya upendeleo kwa  mdogo wao Kalebu(6) ambaye ni mtoto wa mke mdogo wa baba yao.
‘’Chanzo cha mauaji hayo kimebainika, mtoto wa mke mkubwa wa Diwani, Enock amekiri kuhusika na mauaji hayo ameshirikiana na nduguye Gabriel Simwelu, madai yao, baba yao amemwandikisha mali zote marehemu Kalebu, mtoto wa mke mdogo wa Diwani,’’amesema Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Barakael Masaki katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi kwa Vyombo vya habari iliyotolewa na Kamanda Masaki ni kwamba mmoja wa watuhumiwa walioshikiliwa kwa ajili ya mahojiano ambaye ni kaka wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Enock Simwelu(23) amedai kukiri kufanya mauaji hayo akishirikiana na mdogo wake aliyemtambulisha kwa jina la Gabriel Simwelu(19).
Kulingana na taarifa hiyo ni kwamba mtuhumiwa huyo alidai kuwa yeye amehusika moja kwa moja na mauaji hayo kutokana na tatizo la baba yake kuandikisha mali zote kwa mdogo wao ambaye ni mtoto wa mke mdogo Kalebu Simwelu.
Kamanda Masaki alisema kuwa mauaji hayo pia yalifanywa kwa kushirikiana na jirani na rafiki yao aliyefahamika kwa jina la Patrick Msigwa(18) mkazi wa eneo la Majengo katika mji mdogo wa Tunduma.
Mara baada ya kutokea kwa mauaji hayo Jeshi la Polisi liliwanasa watu watano wakiwemo watoto wa mke mkubwa wa Diwani Simwelu ambapo kulingana na madai ya awali ni kwamba chanzo kilitokana na mgogoro wa kifamilia.
Wakati tukio hilo la mauaji linatokea Baba wa marehemu Simwelu alikuwa shambani katika kijiji cha Kipaka ilhali mama mzazi wa mtoto Tumaini Yohana(29) alikuwa kazini katika Ofisi ya Halmashauri ya mji wa Tunduma.
Aidha mazishi ya mtoto Kalebu yalifanyika Disemba 21 kwenye makaburi ya Nakonde katika mji mdogo uliopo nchini Zambia na kuhudhuria na umati wa wakazi wa mpakani mwa Tanzania na Zambia ambapo mwili wa mfanyakazi wa ndani Sista Nyirenge yalifanyika katika kijiji cha Isansa wilayani Mbozi.(PICHA KWA HISANI YA SHOMI MTAKI-TUNDUMA) PAMOJA NA RASHID MKWINDA BLOG

TAARIFA YA YANGA YA KUSITISHA MKATABA WA KOCHA WAKE MHOLANZI BRANDTS


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhbE15WHhTj1r0NP6sBGQaY2dcPq0jAxbq0tGA0sOKQp7xQTqFkNwLfZZH2z1UZ2gcX488pP5L1HNnDtq_iA8nmsYjBn16PKQflLM7jwXC-htSsWem7V1ocrNjgNSINPHKeeTvlAFXsR_Wy/s1600/BIN+KLEB.jpg
UONGOZI wa klabu ya Young Africans SC umempatia taarifa (Notice) ya siku ya thelathini (30) kocha mkuu mholanzi Ernie Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.
 
Maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.
 
Hatua ya Young Africans SC kusitisha huduma na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo mazuri katika Mashindano yanayotukabili.
 
Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC na wapinzani wetu, na soka tulilocheza kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki kwa kweli ni dhahiri mwalimu amefikia mwisho kimbinu na hana njia mbadala.
 
Young Africans SC imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi.
 
Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30, Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika.
 
Ikiwa Brandts ataondoka mapema timu itaendelea na mazoezi kama kawaida katika kila siku asubuhi katika uwanja wa bora kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi Fred Felix “Minziro”.
 
Ili kuhakikisha timu inafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa uongozi unakamilisha maandalizi ya safari ya kambi nje ya nchi na taratibu zote zitakapokamilika tutawajulisha.
 
Aidha uongozi upo katika mchakato wa kumapata mrithi wa Brandts ambaye ataungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili na Mashindano ya klabu Bingwa Afrika.
 
Mwisho tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga wasivunjike moyo kufuatia matokeo ya bonanza mwishoni mwa wiki, uongozi unajipanga kuhakikisha timu inaimarika kwenye benchi la ufundi na kurudisha furaha katika mzunguko wa pili wa VPL.

Abdallah Bin Kleb
Mwenyekiti - Kamati ya Mashindano
Young Africans Sports Club.
DAR ES SALAAM
23 Disemba, 2013

Friday, December 20, 2013

HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUA,OKWI ATUA DAR NA KUPATA MAPOKEZI MAKUBWA

Okwi akizungumza na Waandishi wa Habari
Anatoka kuelekea kwenye gari
Anasindikizwa na Polisi
Ndani ya gari kiti cha nyuma na Katabaro
Dereva Seif Magari anaondoa gari 'mdogo mdogo' (PICHA KWA HISANI YA BIN ZUBEIR)
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi amewasili jana mchana majira ya saa 9:45 katika uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyererer akitokea nchini Uganda kwa shirika la ndege la Rwanda Air.


Okwi amekuja kujiunga na timu yake mpya Yanga SC ambayo ataanza kuitumikia katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya Kimataifa.
Mara baada ya kuwasili JK Nyerere Okwi alipokelewa na vipngozi wa kamati ya mashindano sambamba na washabiki, wapenzi na wadau wa soka kwa ujumla.
Okwi akiongea na waandishi wa habari uwanja wa ndege amesema anashukuru kwa kufika salama jijini Dar es Salaam na hasa katika timu yake mpya ya Yanga.
Kikubwa ameahidi kucheza kwa uwezo wake wote kuhakikisha anaisaidia timu yake mpya kufanya vizuri katika mashindano yote.
Okwi mara baada ya kuwasalimia washabiki na wanachama wa Yanga uwanja wa Kaunda moja kwa moja ameungana na wachezaji wenzake katika kambi iliyopo Protea kujiandaa na mchezo wa jumapili.

KIMBUNGA KILICHOAMBATANA NA MVUA KALI CHAUA WAWILI NA KUHARIBU NYUMBA ZAIDI YA 183 MBARALI MBEYA


Mkuu wa mkoa Mbeya Abas akielezewa jinsi kimbunga hicho kilivyo haribu nyumba za wananchi wa kata tatu Mbarali




Mkuu wa mkoa Mbeya akitembelea maeneo yalioadhirika na kimbunga hicho

Moja ya waadhirika katika kimbunga hicho








HABARI KAMILI TUTAWALETEA HAPO BAADAE


Picha na Mbeya yetu

ANGALIA PICHA ZA AJALI LA BASI LA HOOD MKOANI MOROGORO PAMOJA NA BAADHI YA VIUNGO VYA WATU

BASI LA HOOD LIKIWA LIMEANGUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA MTU MMOJA NA WENGINE WENGI KUPOTEZA BAADHI YA VIUNGO VYAO ENEO LA MELELA MKOANI MOROGORO,BASI HILO LILIKUWA LIKITOKEA MBEYA KWENDA ARUSHA

BASI LA HOOD LIKIINULIWA NA CRANE

MMOJA WA WAOKOAJI AKIWA AMESHIKA KIPANDE CHA MGUU CHA MMOJA WA ABIRIA KILICHOKATIKA KATIKA AJALI HIYO

MIZIGO YA ABIRIA IKITOLEWA KWENYE BASI


Tuesday, December 17, 2013

PICTURE OF THE DAY:BOYS TWO MEN ANA KWA ANA MONDULI



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole na kumrekebisha tai mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa ambaye juzi alinusurika katika ajali ya ndege baada ya ndege aliyokuwa akisafiria  inayomilikiwa na Shirika la Ndege ya Precision kupasuka matairi yote ya nyuma wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa mjini Arusha. Rais Kikwete alikuwa Monduli Mkoani Arusha kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi la Wananchi wa Tanzania katika chuo cha jeshi Monduli.

AJALI YA TRENI NA GARI ENEO LA HAZINA DODOMA

GARI LILILOGONGANA NA TRENI ENEO LA HAZINA DODOMA

ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI WAKITAFAKARI JAMBO BAADA YA AJALI

ENEO LA TUKIO HUKU BAADHI YA WATU WAKIPIGA PICHA NA DEREVA WA GARI HILO ALIJERUHIWA VIBAYA

Monday, December 16, 2013

MIUNDOMBINU MIBOVU JIJINI DAR HUONEKANA PINDI MVUA ZINAVYONYESHA,TAZAMA PICHA HIZI ZILIVYONASWA NA CAMERA YETUP





PICHA NA MAULID KAMBAYA

BOMOA BOMOA YA TANROADS KUPISHA UTANUZI WA BARABARA TABATA AROMA

WANANCHI WAKIKISHANGAA KIJIKO KILICHOKUWA KINABOMOA BAADHI YA NYUMBA MITAA YA TABATA AROMA

UBOMOAJI UKUENDELEA

BAADA YA KUBOMOLEWA

MAOFISA WA TANROADS WAKISIMAMIA ZOEZI

KATAPILLA LIKIFANYA KAZI YAKE MITAA YA TABATA AROMA

KAZI IKIENDELEA(PICHA NA MAULID KAMBAYA)

AJALI KATIKA DARAJA LA MLALAKUA

MTU AMBAE HAKUFAHAMIKA JINA LAKE MARA MOJA ANAONEKANA AKIELEA JUU YA MTO MARA BAADA YA KUPATA AJALI KATIKA DARAJA LA JKT MLALAKUWA NA KUPOTEZA MAISHA PAPO HAPO PEMBENI YAKE NI GARI ALOKUWA NAYO

TAZAMA PICHA ZA MATUKIO MBALI MBALI KWENYE MAZIKO YA MZEE MANDELA

WINNIE NA CLACA MACHEL

JENEZA LA MZEE MANDELA LIKIWA TAYARI LIMESHUSHWA KABURINI


MSAFARA WA KUELEKEA MAKABURINI





RAIS WA AFRICA KUSINI JACOB ZUMA KATIKA MAJONZI WAKATI JENEZA LA MZEE MANDELA LIKISHUSHWA KABURINI

RAFIKI MKUBWA WA MZEE MANDELA NA MPINGA UBAGUZI WA RANGI AHMED KATHRADE AKIZUNGUMZA NA RAIS MSTAAFU WA NCHI HIYO THABU MBEKI



TARATIBU ZA KIMILA ZIKIFANYIKA AMBAPO BENDERA YA NCHI HIYO ILITOLEWA NA JENEZA KUFUNIKWA NGOZI YA NG'OMBE




WINNIE NA CLACA


WAKATI MGUMU WINNIE NA CLACA WAKIWA NA MAJONZI TELE



RAIS JAKAYA KIKWETE ALIPATA FURSA YA KUHUTUBIA KABLA MZEE MANDELA HAJAZIKWA

RAIS MSTAAFU WA ZAMBIA KENETH KAUNDA NAE ALIPATA FURSA YA KUMZUNGUMZIA MZEE MANDELA

KENNETH KAUNDA


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...