Aida
Nakawala mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya,
hivi karibuni alijifungua watoto wanne mapacha kwa mkupuo(Quadliplets)
katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.
|
kikosi cha blog ya www.mbeyayetu.blogspot.com Kikiongozwa na Joseph Mwaisango ambacho kilifika kumjulia hali kiliguswa na hali hiyo na kujitolea kamsaada kidogo wa nguo za watoto sabuni chupa na dishi hivyo kuwaomba wadau wengine kumsaidia mama huyo ili aweze kuwalea vizuri watoto wake. |
Katibu msaidizi wa hospitali ya Rufaa Mbeya Mwansasu akipokea msaada huo kwa niaba ya mzazi |
KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida
Mwanamke mmoja, Aida Nakawala mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa
wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne mapacha kwa mkupuo(Quadliplets)
katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.
Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa
anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake
wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi
Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa
kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.
Kwa mujibu wa Muguuzi wa Hospitali ya
Wilaya ya Mbozi aliyemfanyia huduma mwanamke huyo, Grace Konga alisema mzazi
huyo ni miongoni mwa wazazi 9 waliojifungua katika Mkesha wa Mwaka mpya huku
yeye akivunja rekodi kwa kujifungua watoto wanne kwa njia ya kawaida.
Muuguzi huyo alisema watoto hao
walizaliwa wakiwa na uzito uliotofautiana kwa mtoto wa kwanza hadi wa
mwisho kuanzia kilogramu 1.6,1.5,1.5 na 2.0 ambapo baada ya kuona
hali hiyo ilibidi kumpa rufaa kwa ajili ya msaada zaidi katika Hospitali ya
wazazi ya Meta ambapo wapo katika Chumba cha Joto hadi sasa.
Aidha kwa mujibu wa Muuguzi na msimamizi
wa Watoto katika chumba cha Joto Sista Frolence Maisa amesema hali za watoto ni
nzuri ambapo mama mzazi anahitaji kupatiwa vyakula vinavyoweza kumuongezea
maziwa mengi kutokana na idadi ya watoto aliyonayo.
Alisema kwa hivi sasa watoto wananyonya
vizuri amb po maziwa yakipungua kwa mama itahitajika msaada wa maziwa ya
Kopo aina ya Laktojeni ili watoto waendelee kupatiwa maziwa kama kawaida na
afya zao kuimarika.
Kwa upande wake Mzazi wa watoto hao Aida
Nakawala alisema hali yake kiuchumi siyo nzuri kuweza kumudu kuwalea watoto hao
na kuongeza kuwa mume wake ni mkulima aliyemtaja kwa jina la Web Simkanda hivyo
anaomba msaada wa hali na mali kutoka kwa wasamaria wema.
Alisema huo ni uzao wake wanne ambapo
mtoto wake wa kwanza anaumri wa miaka saba, anayefuata ana miaka miwili na
miezi tisa huku mwingine akiwa amefariki dunia mara baada ya kujifungua kabla
ya uzao huu unaofanya kuwa na watoto Sita.
Alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa hali kama
hiyo ya kujifungua watoto zaidi ya mmoja katika familia yao alisema Mama yake
mzazi amewahi kujifungua mapacha wawili tu na hakuna mtu mwingine aliyewahi
kuzidisha idadi hiyo ya watoto kama yeye.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment