Monday, January 13, 2014

BIBI MMOJA ABAKWA NA VIJANA ENEO LA CHANIKA



chumba cha bibi huyo



sehemu ambapo bibi huyo alibakwa

nyumba anayoishi bibi huyo




akipakiwa kwenye piki piki kukimbizwa hospitali

Bibi mmoja jina tunalihifadhi amevamiwa na kubakwa nyumbani kwake maeneo ya Chanika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam wakati amelala.

Mashuhuda wa tukio hili wanasema bibi huyo alivamiwa na kundi la vijana nyumbani kwake usiku wakati nyumba ya pili tu anakokaa bibi huyo kulikuwa na kigodoro ambapo wakazi wa maeneo mbali mbali hapa jijini hukesha kwa kucheza ngoma na muziki usiku kucha.

Vijana hao walipovunja mlango wa bibi huyo wakamtoa hadi kwenye korido yake na mmoja wapo akambaka na kumlawiti wengine wakakimbia kwa kuhofia kukutwa.

Baadae wakamuacha bibi huyo akiwa akiugulia maumivu,na badala ya kumpeleka hospitali kuna jirani akawa anamkanda tu nyumbani hadi majirani walipogundua hali hiyo ndiyo wakampakia kwenye piki piki na kumkimbiza hospital.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...