Friday, January 10, 2014

MESSI AREJEA KWA KISHINDO ATUPIA MBILI DHIDI YA GETAFE

Back in action: Lionel Messi celebrates scoring on his return from injury in the Copa del Rey clash with Getafe
Messi akishangilia goli baada ya kurejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi.

On strike: Messi strikes the ball to score after returning from a spell on the sidelines with a thigh injury
 Messi akifunga goli mara tu aliporejea uwanjani baada ya kukaa nje ya uwanja kutokana na kupata majeraha ya paja,messi alitupia mbili kati nne dhidi ya getafe.

 Lionel Messi amefunga mabao mawili akiwa amerejea baada ya kukaa nje kwa miezi miwili akisumbuliwa na tatizo la misuli na kuisaidia Barcelona kuichapa Getafe 4-0 katika mchezo wa kwanza wa raundi ya tano ya Kombe la Mfalme.

Tangu alipoumia Novemba 10 mwaka jana, Messi aliingia uwanjani kwa mara ya kwanza kuchukua nafasi ya Andres Iniesta alifunga bao lake la kwanza dakika ya 61 na ya 87 akimalizia kazi ya Martin Montoya. Hilo lilikuwa ni bao lake la 16 na 17 msimu huu.

‘’Nilijisikia vizuri wakati wa mazoezi pamoja na kuwa walinifanyia vipimo lakini unapoingia uwanjani kila kitu kinakuwa tofauti,’’ alisema Messi na kuongeza. ‘’Mwili wangu upo safi kabisa, sijahisi maumivu yoyote ya misuli.’’

‘’Nilicheza nikiwa ni majeruhi,’’ alisema Messi ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa siku 59.

‘’Lakini nashukuru nimefanikiwa nimepona na sasa nimeanza vizuri mwaka huu.’’

Mwanasoka huyo bora mara nne wa Fifa alikosa mechi 12 za msimu huu kwa sababu ya kuumia.

Cesc Fabregas aliifungia Barcelona bao la kuongoza dakika ya saba na kupachika la pili kwa mkwaju wa penalti  61, likiwa ni bao lake la 11.

Mechi ya marudiano dhidi ya Getafe itafanyika Januari 16.

Real Betis inayoshika nafasi ya mwisho katika Ligi ya Hispania, iliichapa Athletic Bilbao, nayo timu ya daraja la pili ya Alcorcon ilishinda 1-0 dhidi ya Espanyol huku Racing Santander wakitoka sare na Almeria.

Manchester City iliisambaratisha West Ham 6-0 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Ligi, huku Alvaro Negredo akifunga mabao matatu.

Hicho ni kipigo cha pili kikubwa kwa West Ham ndani ya siku nne.

Edin Dzeko alifunga mabao mawili na Yaya Toure moja kwa City, inayosaka kucheza fainali ya Kombe la Ligi kwa mara ya kwanza tangu walipofanya hivyo mwaka 1976.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...