Monday, February 10, 2014

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA WATU TISA MKOANI MARA AFARIKI DUNIA

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA WATU TISA MKOANI MARA BW CHARLES KICHUNE MARA BAADA YA KUTIWA MBARONI

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA WATU TISA AMBAE NAE SASA NI MAREHEM BW CHARLES KICHUNE


AKIWA CHINI YA ULINZI MKALI ILI WANANCHI WAMUONE
Mtuhumiwa ya mauaji ya watu tisa na unyang'anyi wilaya ya Tarime mkoani mara,aliyekuwa akihojiwa na polisi kwa tuhuma zilizokuwa zinamkabili,amefariki dunia katika hospitali ya wilaya wakati akipatiwa matinbabu ya ugonjwa wa pumu.

Kamanda wa polisi Tarime na Rorya kamishna msaidizi wa polisi Justus Kamugisha,amesema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halisi ni Charles Kichune(38),alifariki usiku wa kuamkia jana wakati akipatiwa matibabu ya ugonjwa huo wa pumu.

Majina mengine aliyokuwa anayatumia  kwa mujibu wa kamanda Kamugisha ni pamoja na Josephat Chacha na Charles Msongo.

Amesema mwili wwake upo katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ukisubiri kufanyiwa uchunguzi na kuchukuliwa na ndugu zake.

Baadhi ya raia waliouawa ni pamoja na David Yomam,Samuel Matiko,Robert Machimbe,Zakaria Marwa,Juma Nyaitare,Juma mwita,Marwa Mwita na Erick Makanya.

Kwa Mujibu wa Kamanda Kamugisha,Kichune baada ya kukamatwa na kuhojiwa na polisi alikiri kuhusika katika mauaji ya watu mbalimbali katika kata za Binagi,Turwa na Kitare katika vijiji vya Mogabiri,Kenyamanyori,Nkende na Rebu.

 KUHUSU KUKAMATWA KWAKE

Awali kamanda Kamugisha alitangaza kuhusu kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na alisema kwamba,“Mtu huyu amekamatwa mkoani Tanga Februari 6 majira ya saa 1:30 jioni. Hata hivyo hakuwa na silaha yoyote ndani ya begi lake la nguo. Takribani raia 9 wameaga dunia kwa kuuawa na mtu huyu, ambaye amekiri kuhusika na matukio hayo yote.

“Baada ya kumweka chini ya ulinzi na kuanza kumhoji, ndipo tukagundua kuwa si yeye peke yake anayefanya matukio haya bali wako wengi japokuwa aliyekuwa akifahamika ni yeye tu,” alisema.

Kamanda Kamugisha alisema, alipohojiwa zaidi mtu huyo alieleza ilipo silaha anayoitumia na kuwaomba askari kuwapeleka alikokuwa ameificha. 

“Polisi mkoani Tanga waliondoka hadi mkoani Mara, ambapo aliwafikisha kwa jambazi mwenzake aliyemwachia baada ya kuona kuwa Jeshi la Polisi limeanza kumtafuta.

“Aliwapeleka maofisa wa Jeshi la Polisi hadi Kijiji cha Bweri Musoma mjini, kwa mwenzake aliyemtaja kwa jina la Marwa Keryoba au Alex anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 na 38, ambaye ni mkazi wa Sirari akiishi Musoma.

“Wakati polisi wanaingia kwa Keryoba, aliwasikia na kutoka nje akiwa amevaa koti refu jeusi kisha kulitupa chini kwa lengo la kupoteza mwonekano wake. 

“Hata hivyo polisi walipiga risasi juu kumtaka ajisalimishe, japo alianza mashambulizi kuwashambulia maaskari hao.

“Askari walimuua Keryoba kwa kumpiga risasi baada ya kukaidi amri ya Jeshi la Polisi, lililomtaka ajisalimishe, kwa vile alikuwa amebeba silaha ya SMG iliyokatwa kitako na mtutu huku imefutika namba,” alisema Kamugisha na kuongeza:

“Baada ya kumpekua walimkuta akiwa na vitu vifuatavyo, SMG iliyofungwa tochi kwenye mtutu, magazine moja yenye risasi kumi na kwenye nyumba aliyokuwa anaishi marehemu zilipatikana simu mbili za mkononi.

“Vitu vingine ni CD 21 za picha mbalimbali, deki moja, viatu pea mbili aina ya buti, tochi mbili na mpira wa baiskeli pamoja na bidhaa mbalimbali za dukani,” alisema.

Kamugisha aliwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kurahisisha utendaji wa kazi wa chombo hiki chenye dhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...