Wednesday, February 26, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00207WATU WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
WATU WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MWAMBEGELE KATA YA KYIMO, TARAFA YA  UKUKWE BARABARA YA  TUKUYU/MBEYA WILAYA YA  RUNGWE. AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 25.02.2014 MAJIRA YA SAA 16:00HRS JIONI BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI  T.873 BZA/T.501 CCZ AINA YA  HOWO TRUCK MALI   YA  CHAINER TRUCK COMPANY LTD LILILOKUWA  LIKIENDESHWA NA DEREVA JOHN MATHIAS @ MWIMBILIZYE (40), MKAZI WA DSM, LIKIWA LIMEBEBA MAKAA YA  MAWE KUTOKA NCHINI MALAWI KUELEKEA DSM KUACHA NJIA NA KUPINDUKA KISHA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WATATU AMBAO NI DEREVA WA GARI HILO, PAMOJA NA WATU WENGINE WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA JINA MOJA MOJA ISAYA, MIAKA KATI YA  43-45, DALALI, MKAZI WA UYOLE  NA SALUM, MIAKA KATI YA  40-42, MSAIDIZI WA DEREVA. PIA MAJERUHI NI HAMISI RAMADHAN (40), DALALI, MKAZI WA UYOLE. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MAKANDANA TUKUYU NA MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALINI HAPO. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA ANAMILIKI SHAMBA LA BHANGI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SPRIANO WILSON (40), MKAZI WA IFUMA AKIWA ANAMILIKI SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA WA ROBO HEKTA LIKIWA NA MICHE YENYE UREFU WA FUTI TATU [03]. MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 25.02.2014 MAJIRA YA SAA 11:30HRS ASUBUHI
HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KAGERA, KIJIJI CHA IFUMA, KATA YA   LUPA, TARAFA YA KIPEMBAWE WILAYA YA CHUNYA. MTUHUMIWA NI MKULIMA/MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOMILIKI MASHAMBA YA BHANGI NA WANAJIHUSISHA NA UUZAJI/USAMBAZAJI WA BHANGI AZITOE KWA JESHI LA POLISI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA MICHE 27 YA BHANGI KATIKA SHAMBA LAKE.
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ISRAEL MWAMBENE (39), MKAZI WA SIMIKE ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA MICHE YA BHANGI 27, YENYE UREFU WA FUTI 2.5 ALIYOKUWA AMELIMA KWENYE SHAMBA LA MIGOMBA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 25.02.2014 MAJIRA YA SAA 12:20HRS MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MALIBILA, KIJIJI CHA SIMIKE, KATA YA  LUFINGO, TARAFA YA  UKUKWE WILAYA YA  RUNGWE. MTUHUMIWA NI MKULIMA/MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOMILIKI MASHAMBA YA BHANGI NA WANAJIHUSISHA NA UUZAJI/USAMBAZAJI WA BHANGI AZITOE KWA JESHI LA POLISI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Signed by:
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...