NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA MALAYSIA BOING 777 ILIYOPOTEA NA MPAKA SASA HAIJULIKANI ILIPO IKIWA NA ABIRIA ZAIDI YA 200 |
WATAALAM WA VIETNAM WAKIWA KATIKA NDEGE KUFUATILIA ENEO AMBALO WANAHISI NDEGE HIYO ILIANGUKA |
SEHEMU HII INAONYESHA MAFUTA YAKIWA YANAELEA WATAALAM WA VIETNAM WANAHISI IMEANGUKIA HAPA |
SEHEMU INAPOHISIWA KUWA NDEGE YA MALAYSIA IMEANGUKA |
WAPENZI HAWA WALIKUWEMO KATIKA NDEGE HIYO NA INAHOFIWA WAMEPOTEZA MAISHA |
MOJA YA FAMILIA YA WATU WALIOSAFIRI NA NDEGE HIYO |
NDUGU WA ABIRIA AKILIA KWA UCHUNGU MARA BAADA YA KUPOKEA TAARIFA YA KUPOTEA KWA NDEGE HIYO |
WAZAZI HAWA MAMA MWENYE SURUALI NYEUSI NA BABA MWENYE JAKETI JEUSI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA KIJANA WAO NA MPENZI WAKE KABLA YA KUONDOKA KUALA LUMPUR NA NDEGE ILIYOPOTEA |
Wataalam wa masuala ya anga wanasema wakati
mgumu na tete kwa ndege yeyote ni wakati inataka kuruka au kutua,mara chache
sana matukio yasiyokuwa ya kawaida huwa yanatokea pale ndege inapokuwa angani
umbali wa takribani mile saba sawa na kilometa 11 kutoka usawa wa ardhi.
Kwa
hiyo kwa kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Malaysi awakati ikiwa
angani siku ya Jumamosi asubuhi ikiwa na abiria zaidi ya 200 katika bahari ya
kaskazini mwa China,imefanya wataalamu wa masuala ya anga kubaini kwamba
chochote ambacho kitakuwa kimetokea basi kitakuwa kimetokea ghafla na kwa
haraka mno kiasi cha kumfanya hata rubani wa ndege hiyo kushindwa kupiga simu
ya dharula.
Inaweza ikachukua miezi au hata
mwaka kwa wachunguzi wa ajali za ndege kubaini kile kilichotokea kwa ndege hiyo
ya shirika la ndege la Malaysia boing 777 iliyoruka kutoka mji mkuu wa Malaysia
Kuala Lumpur kuelekea China.
Mmoja kati ya wachunguzi hao wa
ajali za ndege bw Todd Curtis ambae ni mhandisi wa masuala ya ndege
mstaafu,amesema katika hatua ya awali kabisa ya uchunguzi wao wanajitahidi
kutafuta ukweli wa mambo ambayo mpaka sasa hawayajui.Todd ameshafanya kazi kwenye
ndege hiyo boing 777 na sasa ni mkurugenzi wa taasisi moja ya usalama wa ndege
huko Malaysia Airsafe.com foundation.
Radar ya jeshi imebashiri kwamba
ndege hiyo iliyopotea Boing 777 inaweza kuwa iligeuza safari iliyokuwa imeianza
kabla ya kupotea,Mkuu wa shirika la ndege la Malaysia amesema siku ya Jumapili
kwamba mamlaka inachunguza abiria wanne ambao utambulisho wao unamashaka.Hii
itaonyesha mazingira yalivyokuwa katika dakika za mwisho kabla ndege haijapata
ajali.Mkuu wa shirika la ndege hakubainisha muelekeo wa ndege hiyo kabla ya
ndege hiyo kupoteza uelekeo au ilikwenda umbali gani kabla ya kupotea ila
baadhi ya taarifa zinatafutwa kwa kushirikiana na radar ya mtu binafsi.
Kama zikipatikana taarifa sahihi
kuwa ndege hiyo iligeuza na kurudi ilikotoka kabla ya kupotea,basi kuna
uwezekano mkubwa kuwa ndege hiyo ilikubwa na tatizo kubwa wakati ikiwa angani
lakini maswali mengi yanaibuka kwa nini rubani hakutoa ishara yeyote katika
chumba cha kuongozea ndege ili apate msaada.Kama kulikuwa na matatizo kidogo ya
kiufundi au engine zote mbili za ndege zilizima,rubani lazima angekuwa na muda
wa kupiga radio ya upepo,Kutokupiga kwake radio ya upepo kunatoa picha kwamba
kuna kitu cha ghafla mno kilitokea hadi akashindwa kufanya chochote, alisema
William Waldock ambae anafundisha masuala ya uchunguzi wa ajali za ndege katika
chuo cha Embry-Riddle Aeronautical Arizona.
Inawezekana kuwa aidha lilitokea
tatizo la ghafla au kitu cha haraka kilichosababisha ikaanguka.Baadhi ya
wataalam wanadhani inawezekana pia likawa ni tukio la ugaidi au rubani akawa
ameiangusha kwa makusudi.
Haijalishi tukio hili limetokea kwa
namna gani,lakini ni mapema mno kusema kitu halisi kilichotokea,Kitu cha msingi
ni kusubiri mabaki ya ndege hiyo yatakapopatikana na kupatikana kwa kisanduku
kinachohifadhi sauti na uchunguzi wa tatizo.Wachunguzi wa kimarekani kutoka
FBI,Bodi ya usafiri Salama ya taifa na shirikisho la uongozi wa anga, na
wataalam wa ndege aina ya Boeing wote wameelekea Asia kusaidia uchunguzi huo.
Utafutaji wa hali ya juu
umeshafanyika baharini lakini mpaka sasa hakuna taarifa yeyote iliyothibitishwa
kupatikana kwa ndege hiyo,ingawa Serikali huko Vietnam imesema kuwa Jumapili
jioni ndege yao ilikuwa inapita chini chini katika bahari iliona kitu kama cha
pembe tatu kilomita karibu 90 sawa na mile 56 kusini mwa kisiwa cha Tho
Chu,sehemu hiyo hiyo ambayo mafuta yameonekana yakielea siku ya Jumapili,lakini
gazeti la serikali limesema mkuu wa jeshi msaidizi wa Vietnam amekaririwa
akisema kitu hicho kilichoonekana baharini ni mlango wa ndege.
Baadhi ya mambo yanayohisiwa kuwa
yamesababisha ndege hiyo kupotea ni muundo wa umbo la ndege ambao ni
Alluminium,hali mbaya ya hewa,Rubani kutotambua tatizo mapema,kuzima au
kushindwa kufanya kazi kwa ingini zote mbili za ndege,kupigwa bomu au kutekwa
hizi ni baadhi ya sababu zinazohisiwa na wataalamu wa ajali za ndege na usalama
wa anga kuwa zimesanbabisha ndege hiyo kupotea.
No comments:
Post a Comment