BAADHI YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA AJALI HIYO |
HALI ILIVYOKUWA ENEO LA AJALI |
MOJA YA BASI LILOHUSIKA KATIKA AJALI |
HII NDIYO HALI HALISI ENEO LA AJALI |
ENEO LA AJALI |
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema imetokea wakati dereva wa gari la abiria lililokuwa likielekea Mwenge kutoka Tegeta ambaye alikuwa katika mwendo wa kasi kubwa kushindwa kulimudu gari lake na kusababisha kuhamia upande wa pili wa barabara na kuligonga basi lingine la abiria lililokuwa likitokea Mwenge kuelekea Tegeta.
Akielezea ajali hiyo,kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa kipolisi kinondoni kamanda AWADH HAJI amesema ajali hiyo ilitokea saa saba mchana na kuhusisha magari manne moja likiwa la raia wa China ambalo liliwakanyaga majeruhi na kuwaua sita kati yao.
Mganga Mkuu wa hospiitali ya jeshi Lugalo ambako maiti na majeruhi walipelekwa brigedia jenerali Dr Makere Josiah amethibitisha kupokea majeruhi kumi na wawili na maiti sita huku wengine hali zao zikiwa mbaya na kukimbizwa hospitali ya taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.