Saturday, June 21, 2014

WATU SITA WAMEFARIKI PAPO HAPO KATIKA AJALI BARABARA YA BAGAMOYO ENEO LA MAKONGO JIJINI DAR ES SALAAM

BAADHI YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA AJALI HIYO

HALI ILIVYOKUWA ENEO LA AJALI

MOJA YA BASI LILOHUSIKA KATIKA AJALI

HII NDIYO HALI HALISI ENEO LA AJALI

ENEO LA AJALI

Watu sita wamekufa papo hapo na wengine 12 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne yakiwemo mawili ya abiria iliyotokea eneo la Makongo barabara ya bagamoyo jijini Dar es Salaam leo saa saba mchana.

Walioshuhudia ajali hiyo wamesema imetokea wakati dereva wa gari la abiria lililokuwa likielekea Mwenge kutoka Tegeta ambaye alikuwa katika mwendo wa kasi kubwa kushindwa kulimudu gari lake na kusababisha kuhamia upande wa pili wa barabara na kuligonga basi lingine la abiria lililokuwa likitokea Mwenge kuelekea Tegeta.

Akielezea ajali hiyo,kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa kipolisi kinondoni kamanda AWADH HAJI amesema ajali hiyo ilitokea saa saba mchana na kuhusisha magari manne moja likiwa la raia wa China ambalo liliwakanyaga majeruhi na kuwaua sita kati yao.

Mganga Mkuu wa hospiitali ya jeshi Lugalo ambako maiti na majeruhi walipelekwa brigedia jenerali Dr Makere Josiah amethibitisha kupokea majeruhi kumi na wawili na maiti sita huku wengine hali zao zikiwa mbaya na kukimbizwa hospitali ya taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...