Askari
wa Jeshi la Kenya wakiwa eneo la tukio wakijaribu kutoa msaada katika
Ndege ya mizigo iliyoanguka leo asubuhi katika eneo la Utawala kwenye
Uwanja wa Jomo Kenyatta, jijini Nairobi.
Taarifa
kutoka Kenya zinasema kuwa mpaka sasa imefahamika kuwa jumla ya watu
wanne akiwamo Rubani, waliokua kwenye ndege hiyo wameripotiwa kufa baada
ya ndege hiyo kuanguka dakika chache tu baada ya kupaa kutoka kwenye
uwanja huo ikielekea Moghadishu, Somalia.
Ajali
hiyo imetokea alfajiri ya leo ambapo imeelezwa kuwa ndege hiyo ilikua
iondoke mapema kusafirisha zao la Mirungi na bidhaa nyinginezo kuelekea
Somalia.
Akithibitisha
ajali hiyo Mkuu wa Polisi wa Jiji la Nairobi, Benson Kibue, amesema
kuwa kuwa Ndege hiyo yenye nambari 5Y-CET ilianguka kwenye paa la jengo
la kibiashara wakati likijaribu kutua ghafla baada ya kutokea hitilafu
katika ndege hiyo na kushika moto kisha kuanza kuteketea na watu wanne
waliokua ndani.
Aidha
kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi wa Jijini Nairobi, Benson Kibue, amesema
kuwa katika ajali hiyo walinzi wawili walijeruhiwa mmoja ametibiwa na
kuruhusiwa kurejea nyumbani huku mmoja akilalazwa katika hospitali ya
Mama Lucy.
Polisi wanaendelea na uchunguzi kwenye mabaki ya ndege hiyo kuona iwapo kuna waathirika zaidi.
No comments:
Post a Comment