Thursday, February 21, 2013

AMA KWELI MSONDO NGOMA WALISHASEMA UKIONA MTU MZIMA ANALIA BASI UJUE KUNA JAMBO...

Pole sana bwana mzee ndo ukubwa huo

SHILOLE ATUA SOUTH AFRICA NA KUSHUSHA BONGE LA SHOW

Shilole kabla ya kupanda jukwaani kufanya vitu vyake
kabla ya kwenda ukumbini kufanya mambo yake
akiwasiliana na jamaa kama mambo yanaenda sawa ukumbini
hapo sasa shughuli ilianza
akiwapagawisha mashabiki na miuno
ukinipa utataka tena,tena na teeenaa........................
mashabiki wakizidi kupagawa


Wednesday, February 20, 2013

MTENDAJI MKUU WA BANK YA STANDARD CHARTERD ATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI VYA IPP PAMOJA NA UJUMBE WAKE NA KUJIONEA JINSI VINAVYOFANYA KAZI

Mussa Jallow,Juanita Mramba mwenye blue na Chip G Kunze maafisa kutoka bank ya standard charterdwakiskiza kwa makini maelezo khusu utayarishaji wa vipindi
Sophia na Nasser wa EATV wakitoa maelezo  kuhusu namna kituo hicho kinavyofanya kazi
Macharia Koigi mkurugenzi wa ITV,akitoa maelezo kwenye blue studio namna inavyotumika,kulia kabisa ni mtendaji mkuu wa standared charterd bank Liz Lloyd akifuatilia maelezo kwa makini.
Mkurugenzi mtendaji wa ITV/Radio One Joyce mhaville akiwa na mtendaji mkuu wa bank hiyo Liz Lloyd na maofisa wengine  wakifuatilia maelezo kwenye moja ya vyumba vya matangazo
Mkurugenzi mtendaji wa ITV/Radio one Joyce Mhaville akitoa maelezo kwa mtendaji mkuu wa bank ya standard charterd Liz Lloyd jinsi vyombo vya habari vya IPP vinavyofanya kazi

Mkurugenz Mtendaji wa ITV/Radio one Joyce Mhaville akifurahia jambo na maofisa wa bank ya standard charterd kwenye studio za kisasa za kurushia taarifa za habari ITV.

BINTI KUTOKA MANYARA ADAI KUFANYIWA UNYAMA NA POLISI


 Sara kimario binti anaedaiwa kubakwa na polisi akifanyiwa mahojiano nje ya kituo cha ITV/Radio one mikocheni akiwa hoi kutokana na kushindwa kukaa kwa madai ya kuingiliwa kinyume na maumbile na polisi

 Sara akiwa amelala akiugulia maumivu makali kwa madai yake kuwa alibakwa na polisi

Sara akipandishwa kwenye gari kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu

Binti mmoja amemlalamikia Polisi wakituo cha Oysterbay Jijini Dar es salaam kwa madai ya kumfanyia kitendo cha unyanyaswaji wa kijinsia baada kufika kituoni hapo kupata msaada wa kiusalama juzi Jioni, Binti huyo ambaye alikuwa anaumwa baada ya kuingiliwa kinyume na maumbile alifanyiwa kitendo hicho kwamara nyingine na Polisi wakituo hicho

Blog hii inafuatilia zaidi kujua kama nipolisi ndiye aliye fanya kitendo hicho au mazingira yenye ukweli na tukio hilo, kwani binti huyo alienda kama muitaji msaada nasi mtuhumiwa wakosa lolote,

Akiongea na Blog hii dada huyo ambaye anaitwa Sara Julius Kimario alielezea kuwa tukio la kugeuzwa kinyume na maumbile na Polisi huyo, lililomkuta baada ya kutoroka kwa mama ambaye alikuwa akimtumikisha kwa shuguli za Ngono katika danguro moja huko Mwananyamala Sokoni,

Binti huyo alidai kuwa Polisi huyo alimuahidi ange mnunulia chakula na kumtafutia mahali pakulala lakini haikuwa hivyo bali alimtendea unyama huo na kuondoka zake bila kumpa msaada wowote, binafsi aliamini angeweza kumsaidia kwani alikuwa akiumwa na ananjaa sana

“ Nilikuwa na kaa mwananyamala sokoni ambapo nilikuwa najishugulisha nabiashara za ngono lakini skuwahi kutumika kinyume na maumbile mpaka majuzi hapa nilipo patwa na maumivu makali baada ya kuingiliwa kwanguvu nakupata maumivu ikabidi nitoroke ilikuweza kupata matibabu” Alisema Sara huku alikilia

Sara alifika kituo cha polisi Oyster-bay tarehe 13. Feb. kwaniaya kupata usalama na mahali pakulala kwani alikuwa akilala kituo cha basi Ubungo bila kupata matibabu yoyote

' Niliwahi kwenda kituo cha polisi Kinondoni ambapo nilipewa Arabii ilikuwa tarehe 7 hakuweza kusema niyamwezi wangapi.....ambapo nilienda hospitali ya Mwananyamala nakupata matibabu ambapo nilishonwa lakini sikuwa nimepona kwajinsi nilivyo umia” Alisema Sara

Hapo awali sara alikuwa akiishi Mwananyamala sokoni ambapo amesema walikuwa kwenye danguro wakifanya biashara ya ngono kwa muda wa miaka 14 sasa, nikwa mama mmoja ambaye anajishugulisha na biashara ya madini na kwa muda huo wote hawakuruhusiwa kutoka nje kabisa

“ Huyu mama anajishugulisha na biashara ya madini (Jina kapuni) na alinitoa kwetu kwania yakufanya kazi zandani lakini baada yakufika huku kazi ilibadilika nakuanza kufanya biashara hiyo” alisema

Sara amesema ndani ya Danguro hilo kwa gorofa yajuu wako mabinti 10 lakini gorofa yachini ajui niidadi ya wasichana wangapi wanakaa, pia jengo hilo linalindwa na walinzi wawili na huwa hawatoki zaidi yakuenda kibara zani. Alisema

POLISI AKANA

Kwakutaka ufafanuzi wa tukio hilo, Nilimpigia OCD Mtafungwa wakituo cha Oyster-bay ilikujua juu yatukio hilo. Ocd alionyesha kutojua tukio hilo nakusema kuwa hana taarifa za mtu kama huyo huku akihaidi kufanya uchunguzi watukio hilo

“ Sifahamu kuusu tukio hilo na kwa sasa siko ofisini, lakini nitalishugulikia na kusu swala la huyo binti kufika kituoni sina taarifa za kiofisi kujua kama niyeye unaye mtaja kwa jina ...nipigie baada ya muda nitakuwa ofisini” Alijibu OCD Mtafungwa wa Oyster-bay

Alizidi kueleza, kuna binti ambaye yuko pake kituo anatatizo kama hilo ila sina uhakika kama ndiye unaye mzungumzia, kwakuwa nitaenda ofisini nitakupa taarifa zaidi Alisema

Hatahivyo, Taarifa kutoka kwa mtu wandani wa Jeshi hilo ambaye nitahifadhi jina lake, alinielezea kuwa OCD wakituo hicho alikuwa natarifa za binti huyo pamoja na tukio alilotendewa kwani baada ya kuharifiwa juu yatukio hilo aliomba binti huyo apelekwe kituoni hapo

“Huyo binti tumemrudisha kituo cha Oyster-bay, nakuna taarifa zake za awali nahata danguro hilo alilokuwa akikaa taarifa zake tayari zilishalifikia Polisi wakituo hicho muda mrefu, wanafuatilia” kilisema chanzo hicho

Jeshi la Polisi linadawati lakushugulikia matatizo ya kijinsia ambapo tlimtafuta ilimtafuta mmoja wapo kutoka kituo cha Polisi Kurasini ambaye sitataja jinalake na alikiri kutokea kwa tukio hilo huku akisisitiza hata kama nipolisi hayupo juu ya sheria nakuahidi kulishugulikia tatizo hilo

Kisheria kama wewe ni mtuhuiwa au sio mtuhumiwa unapofika au kufikishwa mikononi mwa Polisi jukumu la usalama wako kwao nilakwanza nasio wao kukudhuru wewe kama ambavyo Sara alivyo fanyiwa unyanyasaji wa kijinsia

Hatahivyo sara alisisitisa zaidi juu yakupata nauli nakurudi kwao, Licha ya maumivu makali anayopata hivi sasa. Sara yuko kituo cha Polisi Oyster-bay.

Monday, February 4, 2013

BAADHI YA MADUKA YATEKETEA KWA MOTO KITUO CHA MWENGE DSM

Baadhi ya maduka katika kituo cha mabasi Mwenge yanateketea kwa moto, ila chanzo cha moto huo bado hakijajulikana. Tutaendelea kukupa taarifa zaidi kadri zitakavyotufikia.

Picha kwa hisani ya blogszamikoa.blogspot.com

HAPPY BIRTHDAY MDAU FATMA ALMASI NYANGASA

Leo ni birthday ya mwandishi na mtangazaji wa ITV Fatma Almasi Nyangasa, nakutakia heri na baraka tele katika siku yako hii maalum.

WIMBO MPYA WA C-SIR MADINI "NDAGU" MSANII KUTOKA MWANZA.

Huu ni wimbo mpya wa msanii kutoka Rock City C-sir Madini unaitwa "NDAGU" ambao amemshirikisha Josefly. Sikiliza na download wimbo huu hapo chini.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...