Takribani
asilimia 28 ya wanafunzi wa kike nchini Afrika Kusini wanaishi na virusi vya
UKIMWI idadi ambayo ni kubwa ukilinganisha na asilimia 4 ya wanafunzi wa kiume
wanaoishi na virusi hivyo. Waziri wa afya wa nchi hiyo Aaron Motsoaledi amesema
wasichana wengi wamekuwa wakiambukizwa kutokana na kushiriki ngono na wanaume
wenye umri mkubwa.
Waziri wa afya wa Afrika kusini Aaron Motsoaledi |
Akitoa takwimu hizo Motsoaledi amesema
wanafunzi wa kike wapatao 94,000 nchini humo wamepata ujauzito katika kipindi
cha mwaka 2011, baadhi yao wakiwa katika umri wa miaka kumi.
Motsoaledi ametoa wito kwa watoto
wote wa kike kutojihusisha kimapenzi na wanaume wenye umri mkubwa na kujiepusha
na ngono ili kupunguza na kasi ya maambukizi ya UKIMWI miongoni mwao.
Taifa hilo lina jumla ya watu
milioni 50, na takwimu za wizara ya afya zinaonyesha watu milioni 6 nchini humo
wanaishi na virusi vya UKIMWI.
Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi
zenye maambukizi makubwa ya UKIMWI duniani, hata hivyo idadi ya vifo
vitokanavyo na ugonjwa huo imekuwa ikipungua siku hadi siku.
Hivi karibuni idara ya afya nchini
humo imeanzisha jitihada za kukabiliana na maambukizi ya VVU kwa watoto wa
shule. Miongoni mwa jitihada hizo ni pamoja na upimaji wa afya kwa hiari na
ugawaji wa mipira ya kufanyia mapenzi
condom
No comments:
Post a Comment