Saturday, March 16, 2013

TOP FLAVOUR KUANZA ZIARA YA KUSAKA VIPAJI MIKOANI



Kundi la muziki wa kizazi kipya lenye maskani yake kigamboni jijini Dar es Salaam limeanza mchakato kwa kusaka vipaji nje ya jiji la maraha Dar es salaam, akizungumza na  Mwaipaya blog mkurugenzi 
wa kundi hilo ambaye pia ndiye mlezi shaaban Ramadhani maarufu kama Sheby alisema kuwa wameamua kufanya hivyo kwakuwa wasanii wengi wa bongo wanafursa kubwa ya kufanya kazi ukilinganisha na wasanii wa mikoani.
Akifunguka zaidi mkurugenzi wa kundi hilo amesema kuwa wasanii watakaopatikana watakuja jijini na kurekodi ngoma moja ambayo itafanyiwa video na kufanyiwa promo na baada ya hapo ngoma hiyo itakuwa ni ya msanii mwenyewe na atakuwa na uhuru nayo.Ziara ya kundi hilo ilianza jana huko mikindani Tanga,leo wapo Lindi na Kesho Mtwara kabla ya kugeuza jijini.

Akizungumzia juu ya kuondoka kwa msanii aliekuwa katika kundi hilo pamoja  produza aliekuwa anakuja kwa kasi sheby alishangaza kidogo baada ya kusema kuwa yeye hamfahamu MAN NGINJA  ambaye alikuwepo ndani ya kundi hilo kwa kudai kuwa aliletwa pale na msanii mwenzake ambaye ni Tony Touch…..’’ huyu jamaa mimi simfahamu ila alikuja hapa na akashiriki katika wimbo wa kundi ambao tuilikopi kwa P square wa beautiful onyinye na alifanya chorus lakini simjui’
Alipoulizwa zaidi vipi kwa upande wa producer wa shebiz records ambaye nae ameondoka muda mfupi tu baada ya kuondoka kwa Man nginja Shebiy alisema kuwa producer huyo alikuwa na mkataba wa kufanya ngoma mbili yaani ngoma moja ya kundi na ngoma moja ya msaniii Tony Touch ya your the one and only aliyomshirikisha mwanadada MEG

Blog hii ililazimika kumtafuta producer Chid Bay ilikuzungumzia hili lakini simu yake ilikuwa haipatikani muda wote ila taarifa ambazo tumezipata ni kwamba kwa sasa mtayarishaji huyo wa mapigo ya muziki anafanya mazoezi ya kuimba na kundi la dansi nchini kundi la Akudo Impact.

Kwa upande wa Man Nginja alipotafutwa yeye  alisema kuwa  anamuachia Mungu na kwamba hata kama kusoma hujui  bac picha unaweza ukaielewa kama ni ya kike au ya kiume na alipotakiwa kuelezea zaidi alisema ipo siku atafunguka ila kwa sasa yupo buzy akiandaa ngoma zake ambapo ameshaachia ngoma moja inayokwenda kwa jina kla kizai Zai alioifanya nje ya kundi la Top fleva.
Mkurugenzi wa kundi la TOP FLAVOUR la kigamboni Shaaban Ramadhan aka SHEBBY

SHEBBY AKICHART

Wasanii wa Top flavour TISTA mwenye rasta Mrs Shebby kati kati na Momba producer wa asahebby's Recordz

Maulid Kambaya akiwa na wasanii wa Top Flavour Tista  na Momba

Maulid Kambaya akifanya mahojiano na Mkurugenzi wa Shebby's Recordz Shaaban Ramadhan kati kati ni Mrs Shebby

Kambaya akiwa na kundi la TOP FLAVOUR mara baada ya Interview

Maulid Kambaya akiwa katika pozi kijiji beach kigamboni mara baada ya kufanya mahojiano na TOP FLAVOUR

Kundi la Top Fleva linaundwa na wasanii wa tatu ambao ni Tony Touch msemaji wa kundi first lady Tista na Momba amabye kwasasa ameshikilia mikoba ya uandaaji wa muziki wa kundi hilo chini ya studio inayomilikiwa na kundi hilo ya Shebiz recods

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...