Saturday, March 30, 2013

MAHAKAMA YA JUU YA KENYA IMERIDHIA USHINDI WA BWANA UHURU KENYATTA KAMA RAIS MTEULE WA NCHI HIYO

Mahakama ya juu ya Kenya kwa kauli moja imeridhia ushindi wa bwana UHURU KENYATTA kama rais mteule wa nchi hiyo kutokana na uchaguzi uliofanyika tarehe nne ya mwezi huu. 
RAIS MTEULE WA KENYA BWANA UHURU KENYATTA NA MGOMBEA MWENZA BW RUTTO

Likitangaza uamuzi wake,jopo la majaji sita likiongozwa na jaji mkuu bwana WILLY MTUNGA,lilitupilia mbali pingamizi tatu zilizodai kuwa matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa na dosari.

Majaji hao wanasema hoja zilizotolewa na walalamikaji akiwemo waziri mkuu bwana RAILA ODINGA,hazikuwa na uzito wa kutosheleza kuyakataa matokeo ya uchaguzi huo ambao Jaji mkuu MTUNGA amesema uliendeshwa kwa uhuru na haki.

Katika uchaguzi huo bwana KENYATTA alipata asilimia 50.07 ya kura wakati mpinzani wake mkuu bwana RAILA ODINGA alipata asilimia 43.25 ya kura

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...