Saturday, March 30, 2013

IDADI YA WATU WALIOKUFA KUTOKANA NA KUANGUKA KWA JENGO LA GHOROFA 16 SASA IMEFIKA 20

Idadi ya watu waliokufa kutokana na kuanguka kwa jengo la ghorofa 16 katika makutano ya mitaa ya Indira Gandhi na Zanaki jijini D ar es Salaam imefikia 20.
MADAKTARI WAKIMPA HUDUMA YA KWANZA MAJERUHI WA AJALI HIYO
HARAKATI ZA UOKOAJI NA UTAFUTAJI WA MIILI YA WAKLIYOPOTEZA MAISHA ZILIVYOKUWA ZINAENDELEA

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam bwana Suleiman Kova,amesema shughuli za utafutaji wa waathiriwa zinaendelea katika eneo la tukio na utambuzi wa maiti unaendelea katika hospitali ya taifa ya Muhimbili na kwamba hadi saa tano asubuhi ya leo maiti wanane walikuwa wametambuliwa na ndugu zao.

Amesema Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuhusika na uzembe   wa ujenzi uliosababisha ghorofa hilo kuporomoka jana asubuhi.

Amewataja wanaoshikiliwa ni pamoja na mmiliki wa kampuni ya ujenzi ya ujenzi ya Lucky Constructions inayomilikiwa na diwani wa kinondoni bwana IBRAHIMU MOHAMED KISOKI.

Amesema baada ya kujiridhisha na uchunguzi kuhusu jengo la pili linalojengwa na kampuni hiyo lililopo mkabala na jengo lililoporomoka huenda jengo hilo likaamriwa kubomolewa.
JENGO LILILOKUWA MKABALA NA LILILOANGUKA LINALOJENGWA NA KAMPUNI ILIYOKUWA INAJENGA JENGO LILILOANGUKA HUENDA LIKABOMOLEWA IWAPO ITABAINIKA NALO LIPO CHINI YA VIWANGO

Watu zaidi ya 60 wanahofiwa kufunikwa kwenye kifusi baada ya jengo hilo lililokuwa linaendelea kujengwa kuporomoka jana saa 2 asubuhi,wakiwemo wajenzi,wapita njia na ombaomba ambao wana mazoea ya kukaa chini ya jengo hilo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...