Monday, April 1, 2013

WATU 18 WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA BAADA YA KUFUNIKWA NA KIFUSI KATIKA MACHIMBO YA MORAM HUKO MOSHONO JIJINI ARUSHA

Watu zaidi ya 18 wanahofiwa wamepoteza maisha baada ya kufunikwa na kifusi katika machimbo ya Moram huko Moshono jijini Arusha.

 Waliokubwa na mkasa huo ni pamoja na wale waliokuwa wanapakia Moram hizo katika malori mawili aina fuso na lingine lenye uzito wa zaidi ya tani 18 ambayo yalifunikwa kabisa na kifusi hicho

Kazi ya uokoaji na utafutaji ya waliopoteza maisha ilikuwa  ikifanywa na askari wa JWTZ wakishirikiana na wadau mbalimbali.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku tatu tu tangu jengo la ghorofa 16 kuporomoka katika makutano ya mitaa ya Indira Gandhi na Z anaki jijini Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu 36 na wengine 17 kujeruhiwa.

MBUNGE WA ARUSHA MJINI MH GODBLESS LEMA AKIWASILI ENEO LA TUKIO

WANANCHI WAKIWA ENEO LA TUKIO KUSHUDIA HALI HALISI YA TUKIO HILO LA KUSIKITISHA

ASKARI WA JWTZ WAKISHIRIKIANA NA WANANCHI KUUBEBA MWILI WA DEREVA WA MOJA YA MALORI YALIYOFUKIWA KABISA NA KIFUSI ENEO LA TUKIO

HALI HALISI ENEO LA TUKIO

WASAMALIA WEMA WAKIMBEBA MMOJA WA WANANCHI AMBAO WALIPOTEZA FAHAMU BAADA YA KUONA MWILI WA RAFIKI YAKE UKITOLEWA KWENYE KIFUSI

WENGINE WALISHINDWA KABISA KUZUIA HISIA ZAO NA KUANGUA VILIO  BAADA YA KUFIKA ENEO LA TUKIO NA KUJIONEA HALI HALISI

SHUGHULI YA UOKOAJI IKIENDELEA

KULIA KABISA NI MOJA YA MALORI YALIYOFUNIKWA NA KIFUSI HICHO NA LINGINE HALIONEKANI KABISA NA KAZI YA KUYAFUKUA HAPO INAENDELEA.(PICHA ZOTE KWA HISANI YA LUKEMUSICFACTORY.BLOGSPOT.COM)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...