MARK ZUCKERBERG FACEBOOK CEO |
MARK AKIWA NA MKEWE PRISCILLA |
RANDI |
Randi Zuckerberg dada yake mark ambaye ni mmoja wa maofisa wa juu wa facebook Inc |
Mark Elliot Zuckerberg alizaliwa May
14,1984,ni mtaalam wa programmes za computer na mjasiliamali wa masuala ya
tovuti wa kimarekani,anajulikana zaidi kama miongoni mwa watu watano waasisi wa
mtandao wa kijamii,facebook. Zuckerberg ni mwenyekiti na mtendaji mkuu wa
kampuni ya mtandao wa kijamii Facebook inc na utajiri wake ambao umetokana na
mtandao huu wa kijamii facebook unakadiriwa kuwa dola za kimarekani bilioni
9.4,na mahesabu haya ni kwa mwaka 2012.
Zuckerberg alizaliwa na kukulia New York Marekani, alianza kujishughulisha na
mambo ya computer akiwa middle school kama hobby tu, kwa msaada wa baba yake na
mwalimu wake aliyependa kumwita Zuckerberg jina la prodigy. Akiwa high
school Phillips Exeter Academy
alipendelea sana fasihi katika lugha.
Baadae akajiunga na Havard College
hapo akachukuwa masomo ya computer science na saikolojia.Akiwa chuoni hapo
aliwahi kubuni mtandao aliouita FACEMASH, ambao uliwawezesha wanafunzi kupitia
mtandao wa chuo kupiga kura.Kutokana na kubuni mtandao huu kupitia mtandao wa
chuo,ulisababisha mtandao huu ufungwe na akachukuliwa hatua za kinidhamu.
Pamoja na wanafunzi aliokuwa anakaa
nao katika chumba kimoja na baadhi ya aliokuwa nao katika chuo kikuu cha Havard
ambao ni Eduardo Saverin, Andrew Mc Collum, Dustin Moskovitz na Chris Hughes
wakaizindua Facebook katika chumba cha bweni lao.Baadae wakaisambaza katika vyuo vingine huko Marekani na mtandao
ukawawezesha wanafunzi kuwasiliana na kutumiana picha kupitia mtandao huu na
kabla hajaenda Palo Alto,Califonia.
Mwaka 2007 Facebook ikampa utajiri
mkubwa na kuwa miongoni mwa mabilionea ulimwenguni akiwa na umri wa miaka 23
tu.Hadi kufikia mwaka 2010 facebook ilikadiriwa kuwa na watumiaji million 500 duniani na hadi kufikia mwaka 2012
facebook imekuwa na watumiaji billion 1,na
kumpa utajiri unaokadiriwa kufikia dola za kimarekani billion 9.4
No comments:
Post a Comment