Sunday, March 3, 2013

RAIS ROBERT MUGABE AFANYIWA BONGE LA PARTY KWA KUTIMIZA MIAKA 89

A
Rais Robert Mugabe akila keki kwenye sherehe yake ya kutimiza miaka 89
Akifurahia maputo yalopambwa kwenye sherehe yake
Akiwa na mkewe kabla ya kukata keki
 
Wafuasi wa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe wamekusanyika katika mji wa Bindura wenye migodi ili kusherehekea rasmi Bwana Mugabe kutimiza miaka 89

Ripoti zinasema sherehe hiyo inagharimu dola 600,000 kutokana na mchango wa makampuni.
Wenye maduka mjini Bindura wanasema waliamrishwa kufunga maduka mapema hapo jana, ili kusaidia kusafisha mji kwa ajili ya party ya siku ya kuzaliwa ya Bwana Mugabe.

Hii ni sherehe ya pili ya Bwana Mugabe kutimiza miaka 89.

Katika party ya kwanza iliyofanywa mwezi uliopita Bwana Mugabe alisema jukumu lake la kuongoza Zimbabwe amepewa na Mungu - ni amri ya Mwenyezi Mungu.

Wapinzani wake wana wasi-wasi kuwa wafuasi wa Bwana Mugabe wanapanga kuanza tena ghasia na vitisho wakati nchi inajitayarisha kwa uchaguzi mkuu utaofanywa mwaka huu.

Wanasema tayari ofisi za makundi yanayochunguza uchaguzi zimeshambuliwa na polisi wamenyang'anya watu mamia ya redio za kuweza kusikiliza matangazo ya mbali.

Zimbabwe itafanya kura ya maoni kuhusu katiba mpya katika majuma mawili yajayo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...