Wednesday, March 13, 2013

MNYAMA AVAMIA UWANJA NA KUZUA TAFRANI

LOIS BENITO AKIKITOA KIMNYAMA HICHO NJE YA UWANJA KABLA HAJAPIGWA MENO
AKIPIGWA JINO LINGINE
BENITO AKING'ATWA NA KANYAMA HICHO
BENITO AKIKIFUKUZA KABLA YA KUKIKAMATA NA KUKITOA NJE YA UWANJA

Mnyama jamii ya panya alizua tafrani uwanjani wakati wa mechi ya mpira wa miguu kwenye michuano  ya Swiss Super League  mchezo kati ya Thun na Zurich.

 Mnyama huyo alikatiza uwanjani kwa mara ya kwanza hali iliyofanya referee  asimamishe kwanza mchezo ila baada ya kupuliza kipyenga kuashiria mchezo uendelee kimnyama hicho kilirudi tena uwanjani hapo ilibidi zitafutwe nyavu kumkamatia ili wamtoe nje ya uwanja, lakini jambo la kushangaza alizichana na akatoka tena kurudi uwanjani, ndipo mchezaji wa Zurich Loris Benito anaeonekana pichani alipoamua kumkimbiza mnyama huyo na kumshika ili amtoe lakini aliambulia kung’atwa kidoleni lakini hakumuachia na akamtoa nje ya uwanja kupisha mchezo uendelee na baadae akapatiwa matibabu ya huduma ya kwanza kwa kujeruhiwa kidoleni, huku kwetu tungesema mambo ya ndumba.Mambo ya kamnyama hayoo!!!!

1 comment:

  1. ingekuwa Bongo; tena zinacheza timu zetu pendwa! hahahaha! pasingekalika!

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...