MH MWIGULU NCHEMBA (MB) IRAMBA MAGHARIBI |
Akichangia hotuba ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu,amesema ana ushahidi wa kutosha juu ya mipango na utekelezaji wa mipango hiyo inayofanywa na baadhi ya wanasiasa kwa manufaa yao binafsi.
Mara baada ya mbunge huyo wa Iramba magharibi kuzungumza,akasimama mbunge wa Mbulu mh MUSTAPHA AKUNAY akitumia kanuni ya bunge ya 68 kifungu cha pili ambacho kinamkataza mbunge kuzungumzia suala lililoko mahakamani na kuomba muongozo wa spika.
Mbunge wa Singida mh TUNDU LISU kwa upande wake amelishutumu jeshi la polisi kwa kupanga ugaidi kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa kisiasa na kisha kuwabambikizia kesi baadhi ya watu.
Kutokana na malumbano hayo,spika wa Bunge Mh ANNA MAKINDA alilazimika kuwataka wabunge kuacha kuyazungumzia au kuyajadili mambo ambayo yako mahakamani,jambo lililopingwa vikali na baadhi ya wabunge,hivyo akaliacha suala hilo lijadiliwe
No comments:
Post a Comment