Friday, May 24, 2013

BAADA YA NGASSA NIYONZIMA ASAINI TENA MKATABA MPYA WA MIAKA MIWILI YANGA

HARUNA NIYONZIMA aka FABRIGAS AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI BAADA YA KUSAINI TENA MKATABA WA MIAKA MIWILI WA KUITUMIKIA TENA CLAB YA YANGA(Picha kwa hisani ya GPL)
Hatimae kiungo wa kimataifa kutoka nchini Rwanda Haruna Niyonzima amefikia makubaliano mapya na timu ya Yanga kwa kusaini mkataba wa  kuitumikia tena timu hiyo yenye maskani yake mtaa wa twiga pale Jangwani.
Awali kulikuwa na tetesi kuwa clab ya simba ilikuwa inamuwania kiungo huyo mwenye chenga na pasi zenye uhakika na zisizomithirika na ilikuwa imemtengea kiasi cha shillingi miliono 70.
Pia tetezi zingine zilivuma kuwa Azam FC nao walimtengea donge nono ili asaini kuichezea timu hiyo.
Kabla ya kusaini mkataba huo leo saa tano asubuhi Niyonzima alishaamua kuondoka kurejea kwao nchini Rwanda kama wangekuwa hawajakubaliana na clabu yake aliyoitumikia kwa mafanikio makubwa msimu uliopita.
Hata hivyo Yanga imemtimizia kila alichokitaka mchezaji huyo hatimae amesaini mkataba huo wa miaka  miwili.
Niyonzima amekuwa mchezaji wa pili kusaini katika club hiyo ikiqwa ni siku chache tu zimepita tangu Mrisho Ngassa nae kusaini mkataba mpya na timu hiyo akitokea Simba.

1 comment:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...