|
MAMA YAKE RAMA |
|
RAMA AKIWA MAHAKAMANI |
|
PICHA YA RAMA NA MAMA YAKE 2008 |
|
PICHA ZOTE KWA HISANI YA GPL |
KIJANA Ramadhan Suleiman Mussa ‘Rama mla watu’ na mama yake
Khadija Ally, leo wameachiwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada
ya kubainika kuwa mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo (mla watu) alifanya
kosa la mauaji akiwa na matitizo ya akili. Hata hivyo Rama Mla Watu, ataendelea
kukaa katika hospitali ya wagonjwa wa akili ya Isanga mkoani Dodoma mpaka akili
yake itakapokuwa sawa ndipo ataachiwa kuwa huru mtaani ili asije akawadhuru
watu wengine. Khadija Ally yeye ameachiwa huru. Rama alijizolea umaarufu
mkubwa mwaka 2008 baada ya kukamatwa akiwa na kichwa cha mtu kinachodaiwa kuwa
ni cha mtoto SaloMahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imeamua kumuachia huru
Ramadhani Selemani Mussa ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya kukutwa na
kichwa cha mtu.
Rama, ambaye muda wote huo alikuwa rumande gereza la Segerea akisota
kusubiri hukumu yake, alikamatwa hospitali ya Muhimbili mwaka 2008 ambapo pia
alikiri kuwa alikuwa na tabia ya kula nyama za watu ambayo amefundishwa
kichawi toka alipokuwa mdogo. Mahakama imemuachia huru kwasababu mtuhumiwa
alitenda kosa hilo pasipo kuwa na akili timamu.
Hata hivyo mahakama hiyo imetoa agizo la
kuendelea kumuweka kijana huyo katika hospitali ya wagonjwa wenye matatizo ya
akili, hospitali ya Isanga iliyopo Dodoma mpaka pale atakapona ndipo aruhusiwe
kurudi mtaaani
sasa hako kaugonjwa alipokuwa segerea kalitulia?maana ugonjwa hauchagui mahala,au alianza matibabu,ila uhuru kapewa sasa,mmm inatisha ugonjwa wa kula watu,GET WELL SOON RAMA.
ReplyDelete