Katikati Redds Miss Kibaha Nzera Kitano , kushoto mshindi wa pili Ester Albert na kulia ni Rachel Joh ambaye ni mshindi wa tatu. |
MISS KIBAHA 2013 NZERA KITANO |
Na Mwandishi wetu
ALIYEKUWA mshiriki namba 6 katika shindano la kumsaka Redds Miss Kibaha 2013 Nzera Kitano ameibuka kua Redds Miss Kibaha 2013 katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Conteainer Kibaha Maili Moja mkoani Pwani.
Nzera ambae alionekana kuwa mchezi tangu mwanzo wa shindano aliweza kupenya katika hatua ya nusu fainali ambapo aliingia katika warembo watano bora kati ya washiriki 10 waliokuwa wakishindana kuwania taji hilo.
Aidha kwa ushindi huo Nzera amepata zawadi ya fedha taslimu sh.300,000 pia amepa ofa ya kwenda kuchagua vipodozi na mapambo ya aina mbalimbali katika duka la Shear Illusion lilipo Mlimani City pamoja na king’amuzi kutoka kampuni ya Multichoice ambapo atafungiwa bure.
Mshindi wa pili ni Ester Albert ambaye amepata fedha taslimu kiasi cha sh.200,000 pia atapata ofa ya kulipiwa ada ya shule au kutafutiwa kazi na mdau ambaye hataki kutaja kwenye vyombo vya habari.
Mshindi wa tatu ni Rachel John aliyepata fedha taslimu sh. 150,000 huku nafasi ya nne ikienda kwa Sylvia John huku nafasi ya tano ilikwenda kwa Beatrice Bahaya.
Kwa ushindi huo warembo wote watano wamepata nafasi ya kwenda kushiriki kwenye shindano la Redds Miss Pwani watakakochuana na warembo wa Bagamoyo kuwania tiketi ya kwenda kushiriki katika shindano la Kanda ikiwa ni katika kuwania tiketi ya shindano la taifa.
Shindano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Linda Media Solution (LIMSO) na kudhaminiwa na
Redds Miss Kibaha ilidhaminiwa na Tanzania Distilleries Konyagi kupitia kinywaji cha Dododma Wine, Redds Premium Cold, Fredito Entertainment, CXC Africa, Michuzi Media Group |(MMG), Aco Catering & Servises, Pr Studio, ASET ,Santorine Holiday Resort na Amazon Night Club.
Bendi ya Muziki wa dansi ya Mashujaa ilitumbuiza na kuwachengua mashabi wa urembo wa mkoa wa Pwani.Washiriki wengine waliobaki walipata kifutajasho cha .sh.100,000 kila mmoja
No comments:
Post a Comment