MCHUNGAJI
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini
Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa mahakamani kungojea kesi yake.
Wananchi Mbalimbali wakisubiri Kusikiliza Kesi ya MCHUNGAJI
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini
Mbeya Daniel Mwasumbi
MCHUNGAJI
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini
Mbeya Daniel Mwasumbi aliye vaa koti Jeupe akiwa anatolewa mahakamani Baada ya kusomewa kifungo cha Miaka 30 Jela
Watoto wa MCHUNGAJI
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini
Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa wanatoka Mahakamani Baada ya Baba yao kusomewa kifungo
Mtoto wa MCHUNGAJI
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini
Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa anaongeaa na waandishi wa Habari baada ya kesi kumalizika
Waumini Mbalimbali wakiwa nje Baada ya kesi kumalizika
Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa nje hawaamini baada ya kusikia Baba yao anafungwa Miaka 30 |
Binti anaye daiwa kufanyiwa kitendo hicho akilia kwa Uchungu baada ya kesi kwisha
***********
Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo amesema Mahakama imemta hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na Shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema Beni(19).
Amesema Mtuhumiwa huyo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mwezi Januari 2008 hadi Mwaka 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na Sheria kifungu cha 130(2)e na 131 (1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kosa la ubakaji.
Kutokana na ushahidi huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mahakama yake imemkuta Mtuhumiwa na makosa mawili ya Ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi uliotolewa na Mhanga mwenyewe pamoja na Mwalimu wa Shule aliyokuwa akisoma ambapo alidai kuwa Shtaka limedhihirishwa pasipo shaka chini ya kifungu cha 235/1985.
Kwa upande wake Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kutokana nan mtuhumiwa kutenda kosa la kinyama tofauti na umri wake na wa binti ambapo Binti anaumri wa Miaka 19 ili hali Mtuihumiwa akiwa na Miaka 57.
Pia alidai kuwa Mtuhumiwa huyo alimwalibia masomo na maisha yake binti huyo na vitendo hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali ikiwemo kanisani hivyo aliiomba mahakama hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya Matunzo ya Watoto kwa kutumia amri ya kutaifisha malishtakiwa.
Hata hivyo Hakimu alimuuliza Mtuhumiwa kupunguziwa adhabu ambapo Mshtakiwa huyo aliomba kupunguziwa adhabu kwa madi kuwa ameachiwa watoto na ndugu zake aliozaliwa nao wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na msaada.
Aidha kutokana na utetezi huo Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo c ha Miaka 30 na viboko 12 kutokana na kosa la kwanza ili hali katika kosa la pili amehukumiwa kifungo cha Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda kwa pamoja na kulipa fidia ya Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania kwa familia ya Mhanga.
Ameongeza kuwa Mtuhumiwa anahaki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu ya Mbeya kama hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa na mahakama yake.
Habari
,Picha na Mbeya yetu Blog
No comments:
Post a Comment