Wednesday, July 3, 2013

TIMU YA MAJIMAJI MKOANI RUVUMA YAPATA UONGOZI MPYA

  Mwenyikiti  wa timu ya  Maji Maji Humphery Millanzi aliyeibuka kidedea kwa ushindi mkubwa katika uchagui wa viongozi wa timu hiyo.
 ..........................
Na Amon Mtega  ,Songea.
TIMU ya majimaji ya wanalizombe mkoani Ruvuma jana imepata uongozi mpya utakao weza kuiongoza timu hiyo kwa muda wa miaka minne.
 
 Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi huo ,Joseph Mapunda uliyofanyika katika ukumbi wa saccos ya walimu uliyopo mjini hapo alisema kuwa kwa nafasi ya mwenyekiti imechukuliwa na Humphery Millanzi kwa kura 89 huku mpinzani wake Mohamed  Issa alipata kura 30.
 
 Mapunda alisema kuwa kwa nafasi ya makamu mwenyekiti mgombea alikuwa ni John Nchimbi ambaye alikuwa mgombea  peke bila upinzani na kufanya apate kura za ndiyo 101huku kura 20 zilikuwa za hapana.
 
 Akifafanua katika nafasi za wajumbe watano alisema kuwa nafasi hizo ziliwaniwa na watu tisa waliyopatikana ni watano nao ni Hilda Kapinga alipata kura 102 Mohamed Matwika kura 99 John Kabisama kura 90 Kitwana  Mzee kura 84 na Salum Masamaki kura 74 .
  
 Aidha alisema kuwa kwa wajumbe walishindwa kupata nafasi hizo ni Joseph Mswila ambaye alipata kura 62 Robarti Mgowole kura 18 Said Mangwe kura 14 na Oddo Mbunda kura 50 huku idadi ya wapiga kura walikuwa 121.
   
 Kwa upande wake mwenyekiti aliyeshinda katika nafasi hiyo Hafrei Milanzi akiongea na chombo hiki alisema kuwa amepongeza ushindi huo huku akiwa ameahidi kushirikiana na wanachama wote wa timu ya majimaji pamoja na wadau mbalimbali ili timu hiyo iweze kusongambele kimchezo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...