Wednesday, July 3, 2013

PAROKO MSAIDIZI WA KANISA KATOLIKI LA MATOGORO AMEWATAKA WAUMINI WA KANISA HILO KUACHA TABIA YA UCHOYO

 

Picha na maktaba



Joyce Joliga,Songea 

WAUMINI wa kanisa katoliki Matogoro Manispaa ya Songea wameshauriwa kuacha uchoyo na badala yake  kujenga tabia ya kusaidiana wao kwa wao bila  kutegemea misaada toka kwa wafadhili wan je ya nchi kwani vitendo hivyo vimepitwa na wakati.

Ushauri huo umetolewa jana na Paroko msaidizi wa kanisa katoriki  la Matogoro Nicolas Mlelwa ambaye amesema,waumini hao wanapashwa kuacha mkono wa birika na wajifunze kusaidiana na kufanya mambo yao wao wenye bila kutegemea wafadhiri.

Amesema,anasikitishwa kuona waumini wa nyanda za juu kusini si watu wa kujitoa tofauti na majimbo mengine ambapo wamekuwa wakiwasaidiana wao kwa wao ikiwa ni pamoja na kuwasaidia mapadri wao
“ Nawaomba waumini muache mkono wa birika, mjenge tabia ya kushirikiana na  muanze kujitegemea kwa kusaidiana nyinyi kwa nyinyi ikiwa ni pamoja na kuwasaidia mapadri wenu kwani kuendelea  kutegemea wafadhili si kitu kizuri bali tuendelee kujitolea kwa moyo wa upendo ,”alisema

Aidha,amewataka waumini hao kuhakikisha wanachangia harambee ya kongamano la vijana wakatoriki ambalo linatarajiwa kufanyika mapema mwezi huu ambapo kiasi kinachotakiwa ni sh 8,000,000 ilikuweza kufanikisha maandalizi yote ya kongamano hilo ambalo litashirikisha vijana wa vyuo vikuu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...