Mama Anabu
Mwambungu Mke wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Na Joyce Joliga,
WANAWAKE
mkoani Ruvuma wameshauriwa kupendana, kushirikiana na kuacha tabia ya
kusengenyana ili waweze kufanikiwa kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja
na kuanzisha vikundi vya ujasiliamali ili viweze kuwasaidia kuinua
kipato chao na familia zao na wasikubali kugombanishwa .
Ushauri
huo umetolewa jana na Mke wa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakati akizindua
rasmi kikundi cha wanawake wajasilimali wanaojishugulisha na ufugaji wa
kuku wa nyama na mayai cha JITIHADA GROUP kilichopo kata ya Lizabon
Manispaa ya Songea.
Amesema,ili
wanawake waweze kufanikiwa kimaendeleo wanapaswa kujenga moyo wa
kupendana kwa dhati , kuaminiana na kushirikiana na kuacha tabia ya
kupigana majungu kitu ambacho kimekuwa kikiua vikundi vingi vya
wanawake .
Anabu ameongeza kuwa ,wanawake wengi wamekuwa wakifanikiwa kuanzisha vikundi ila
vimekuwa havifiki mbali na kuvunjika kitu ambacho si kizuri hivyo
amewataka wanawake kuwa makini na miradi wanayoaanzisha ikiwa ni pamoja
na kushikamana ili waweze kujiletea maendeleo.
“Nawashauri
wanawake wenzangu ,kikundi hiki tukiendeleze ili kiweze kutusaidia
kujikwamua na umaskini kamwe tusikubali kugambanishwa na vijimajungu
vidogo vidogo ,kwani hiyo ndiyo sumu ya vikundi vingi
,mpendane, muaminiane ,mshirikiane na kuvumiliana na mtafika mbali ,
name nawaunga mkono nawachangia kiasi cha sh 200,000,”alisema Anabu
Mwambungu.
Awali
akisoma taarifa ya kikundi hicho Katibu wa Kikundi hicho Theresia Komba
amesema,bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na
kukosa mtaji hali inayowafanya washindwe kuzalisha kwa wingi,pamoja na
ukosefu wa elimu ya ujasiliamali hususani wa ufugaji bora.
Aidha,
wamemwomba Mke wa Mkuu wa mkoa kuwasaidia ili waweze kupata mkopo pamoja
na pembejeo za kilimo ili waweze kuzalisha kwa wingi na kujiongezea
kipato.
No comments:
Post a Comment