Wadau wa kilimo cha mahindi wakiwa katika hatuwa ya mwisho katika mavuno
Na Joyce Joliga
WANANCHI wa
wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wameiomba serikali kuhakikisha inakomesha
tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wa mazao wasiowaaminifu ambao wanapita
kuwarubuni wakulima kwa kubadilishana chakula na simu kitu ambacho
kinawasababishia hasara.
Wakizungumza jana
kwa nyakati tofauti tofauti wamesema kunabaadhi ya wafanyabiashara za mazao
ambao si waaminifu wamekuwa wakipita katika mashamba yao na kuwadanganya kwa
kuwapelekea simu za bei raisi na kubadilishana nao kwa kuwapatia mahindi.
Mmoja wa
wakulima hao Aidan Komba mkazi wa Matiri amesema amejikuta akitoa mahindi dumla
mia sawa na kilo 400 za mahindi baada ya kupewa simu na kuelezwa kuwa inathamani
ya kiasi cha sh 450,000 kitu ambacho kumbe kilikuwa sahihi.
“Tunaomba
serikali itusaidie kuwadhibiti wafanyabiashara ambao wanapita katika maeneo ya
mashambani kwa kuwarubuni wakulima kwa kubadilishana nao vitu vya anasa na
kuchukua mazao yao kwani vitendo hivi vikiachiwa ni hatari na vitatusababishia
njaa,”alisema
Kwa upande wake
Mariam Mahundi mkazi wa Myangayanga Mbinga amesema, alifatwa na mmoja wa
wafanyabiashara wa mazao nyumbani kwake ambapo alimwomba ampatie dumla 30
za mahindi ambapo angempatia simu aina ya Tekno pamoja na memori naye alifanya
hivyo na kukabidhiwa simu hiyo ambapo alipewa maelekezo aichaji masaa sita na
alipomaliza kuchaji aliiwasha ikagoma kuwaka lakini tangu alipochukua simu hiyo
haikufanya kazi na alipoipeleka kwa fundi iligundulika kuwa tayari ilikuwa
imekufa na ilinunuliwa tu kava jipya.
No comments:
Post a Comment