Na Amon Mtega ,Songea na Njombe.
WANANCHI wa tarafa ya Madaba wilaya ya Songea mkoani Ruvuma
pamoja wananchi wa kata ya Mavanga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wameilalamikia
kitengo cha mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Tanzania
[SUMATRA]kwa kuto kuweka wazi bei halali ya viwango vya nauli katika maeneo ya
vijijini hasa kutoka Madaba Songea hadi
Mavanga Ludewa.
Wakiongea na demashonews kwa nyakati tofauti wananchi hao
ambao hawakutaka majina yao yatanjwe gazetini walisema kuwa SUMATRA imeshindwa
kuangalia matatizo ya nauli katika maeneo ya vijijini na kufanya wanamchi kulipa nauli isiyo na kiwango stahiki hata
pakiwa na umbali mdogo lakini nauli ni gharama kubwa.
Wananchi hao waliyokuwepo kituo cha mabasi cha Madaba
wakisubiri usafiri wa kuelekea kata ya Mavanga Ludewa walisema kuwa wanatozwa
nauli ya Tsh 5,000 hadi Tsh 6,000 licha ya umbali wake kuwa ni wa kilometa 44 huku barabara hiyo ikiwa imetengezwa kwa
kiwango cha changarawe na inapitika vizuri .
Wakielezea kiwango
hicho cha nauli walisema kuwa wanashangazwa kuona bei hiyo inalingana na umbali wa kutoka Songea
mjini hadi Madaba ambapo umbali wake ni wa kilometa zaidi ya 120 na kutoka
Njombe hadi Madaba nako umbali unakaribia kulingana kwa kilometa 120 lalkini nauli
zake ni Tsh 5,000 tatizo kwenye kipande kidogo cha barabra kichounganisha wilaya
ya Songea na Ludewa kuwa bei juu bila maelezo ya SUMATRA.
Walisema kuwa kama
SUMATRA imeweza kuweka bayana viwango vya nauli katika maeneo mbalimbali ya
njia kwa kubandika nauli hizo kwenye magari iweje kwa baadhi ya barabara kushindwa
kuwekewa vuwango sahihi vya nauli.
Baadhi yao walitaka
viongozi wa SUMATRA wanao wakilisha mikoa yao ya Njombe na Ruvuma wakutane ili
waweze kulijadili suala hilo kwa kina hasa kwa kiongozi wa mkoa wa Ruvuma kwa
kuwa eneo lake la kutoka Madaba kuelekea Ludewa ni kubwa na linaishia daraja la mto Luhuhu ambalo
linalounganisha pande zote mbili.
Kwa mjibu wa wananchi
hao wamedai kuwa serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha maeneo hayo
yanapatiwa huduma zinazostahiki kama barabara zinazopitika lakini baadhi ya
wamiliki wa vyombo vya usafiri kama mabasi wamekuwa wakikwamisha kwa makusudi na kuwahujumu wananchi kwa kuwapandishia nauli
licha barabara kuwa nzuri.
Kwa upande wake afisa
mfawidhi wa SUMATRA mkoani Ruvuma Denis Daudi akiongea na gazeti hili kwa njia
ya simu amekiri kuwepo kutofanyiwa kazi kiwango hicho cha nauli kulingana na
umbali hivyo ameomba wananchi hilo wapeleke barua ya malalamiko huku yakiwa
yamembatanishwa na risiti zinazonyesha kiwango hicho.
Gazeti hilo lilikuwa tayari kupeleka kieleezo cha risiti kwa
kuwa nalo lilibaini hilo likiwa kwenye msafara huo lakini kiongozi huo alizidi
kuomba ipelekwe kwa maandishi ili ifanyiwe kazi kwa haraka zaidi.
No comments:
Post a Comment