Thursday, July 4, 2013

WANAUME WILAYANI TUNDURU WAWASHITAKI WAKE ZAO HAKI ZA BINADAMU

Picha siyo ya tukio halisi
Na Stevie Chindiye,Tunduru
WANAUME Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma wamewaomba viongozi wa Mtandao wa kutetea haki za Binadamu (Tanzania Human Rights Defenders Coalition-THRDs Coalition) ili uwasaidie kuwapatia mafunzo ya utetezi ili kuwasaidi kujikinga na vitendo vya ukandamizaji ambavyo wamekuwa wakifanyiwa na wake zao.

Ombi hilo limetolewa na Viongozi wa mashirika yasiyo kuwa ya Kiserikali Wilayani humo wakati wakiongea na Viongozi wa Mtandao huo walipotembelea katika Ofisi za Mtandao wa Mashirika ya Kijamii Wilayani Tunduru (MATU) zilizopo Mjini hapo.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima na Wafanyabiashara wa Mazao ya Chakula Tunduru (WAMANATU) Athuman Idd Milanzi ndiye aliyeanza kuvunja ukimya huo kwa kuwaeleza viongozi hao kuwa wanawake wa makabila ya Wayao wamekuwa wakiwanyanyasa waume zao katika utoaji wa maamuzi mbalimbali yakiwemo ya kupeleka watoto wakike katika Unyago. 

Milanzi ambaye aliungwa mkono na Daimu Mnenga aliye kiwakilisha Chama cha Wazee na wastaafu Wilayani humo walidai kuwa pamoja na wake hao kuendesha tabia za ubabe huo pia waliwatuhumu kuwa wanawake hao wamekuwa kikwazo katika maendeleo ya ndoa zao kutokana na kutojali kuachika.

Wakifafanua maelezo hayo walisema kuwa kutokana na wanawake hao kujengeka katika kiburi hicho wakati mwingine wamekuwa hawawahusishi waume zao katika maandalizi ya kuwafunda Watoto wao wa kike hasa ikionekana mwanaume husika haungi mkono taratibu hizo na wakiwa wanadai kuwa mwanamke asiyechezwa hawezi kuishi vizuri na mume atakaye muoa.

Wakiongeaa kwa nyakati tofauti mratibu Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (Tanzania Human Rights Defenders Coalition-THRDs Coalition) Bw. Onesmo Olengurumwa na Afisa Habari wa Mtandao huo Bw. Elias Mhegera ambao pamoja na mambo mengine waliwaahidi kuwapatia mafunzo hayo ambayo walidai kuwa yatawasaidia kujilinda na kutoa utetezi katika matukio ya aina hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...