Na YEREMIAS NGERANGERA----NAMTUMBO
Wakati serikali ikiagiza kuwa uhamisho wa walimu uendane na fedha za kugarimia uhamisho, kuepuka mzigo wa madeni kwa serikali , bado halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma iliwahamisha walimu 25 mwezi januari bila kuwalipa fedha zao mpaka sasa.. Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya walimu hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe kwa ajili ya kuhofia ajira zao walisema kuwa walipata barua za uhamisho mwezi januari lakini chakushangazi waliambiwa walipoti vituo v ipya vya kazi wakati taratibu za malipo yao zinaandaliwa.
( Mimi toka Januari mwaka huu sijafundisha naendelea
kusubiri fedha za uhamisho au gari la kubebea mizigo yangu Kutoka halmashauri
na huu ni mwezi wa sita toka nipate barua ya uhamisho) alisema mwalimu mmoja.
Baadhi ya walimu walidiriki kwenda kwa watu binafsi kwenda kukopa fedha kwa
ajili ya kugharimia uhamisho huo kwa mategemeo ya kupata fedha toka kwa
mwajiri kwa ajili ya kulipia madeni hayo wapo katika hali ya wasiwasi katika
vituo vyao vya kazi kutokana na kero za watu wanaowadai walimu hao. Hata hivyo
kuna baadhi ya walimu ambao hawakutaka kuingia hasara hiyo waliendelea kukaa
nyumbani bila kufundisha kwa miezi sita mpaka shule zinafungwa w akisubiri
fedha za uhamisho.
Katibu wa chama cha
walimu wilayani Namtumbo bwana Werner Mhagama aliwapongeza walimu
walioendelea kusubiri fedha za uhamisho mara tu baada ya kwenda kuripoti
kituo kipya na kurudi kituo cha awali kusubiri fedha za uhamisho au gari la
kubebea mizigo yao kwa madai kuwa walimu hao wapo sahihi kwa kufuata kanuni
za utumishi wa umma. Afisa elimu wa wilaya ya Namtumbo bwana Loberto Mbilinyi
alikiri kuwepo kwa madai ya walimu hao na ku kusema kuwa madai hayo yanalipwa
kwa awamu na baadhi ya walimu walisha lipwa. Mkurugenzi wa wilaya hiyo bwana
Mohamed Maje alisema kuwa uhamisho wa walimu hao ulipita katika vikao halali
kwa kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na bajeti ya malipo kwa walimu hao
ilishafanyika bali pametokea na uchelewaji wa fedha kutoka serikalini..
No comments:
Post a Comment