Wednesday, August 28, 2013

ASKARI WA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI WAJERUHIWA KONGO

Msemaji wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nchini MONUSCO ametangaza kuwa, kwa akali askari watatu wa vikosi hivyo akiwemo mwanajeshi mmoja wa Afrika Kusini, wamejeruhiwa vibaya katika shambulizi la kuvizia lililofanywa na waasi huko mashariki mwa nchi hiyo. Shambulio hilo lilitokea baada ya waasi wa M23 kurusha kombora katika eneo viliko vikosi vya UN umbali wa karibu kilometa nne kaskazini mwa mji wa Goma, makao makuu ya jimbo la Kivu Kaskazini. 

Kwa mujibu wa msemaji wa MONUSCO, askari wengine wawili waliojeruhiwa ni Watanzania. Habari zaidi zinasema kuwa, kwa akali askari wa Afrika Kusini, wameshapambana mara mbili na waasi hao. 

Wakati huo huo, viongozi wa Pretoria, wamekanusha kujiri mashambulizi ya askari wa nchi hiyo dhidi ya waasi wa M23 nchini Congo DRC.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...