Wednesday, August 28, 2013

IRAN INATENGENEZA NDEGE YA KISASA YA KIVITA

Ndege ya kivita ya Qaher-313 iliyotengenezwa Iran na kuzindiliwa Tehran Februari 2 2013

Iran hivi sasa inatengeneza ndege ya kisasa kabisa ya kivita ambayo ni kati ya zana za kijeshi zilizotengenezwa na wataalamu wa hapa nchini.
 
Hayo yamedokezwa leo na Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh, kamanda wa ngazi za juu katika Jeshi la Angani la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIAF).

Amesema utengenezaji wa ndege hiyo utaifanya Iran iache kabisa kutegemea ndege za kivita za kigeni hasa zile ambazo zinatumika kwa ajili ya mafunzo. Ameongeza kuwa Jeshi la Iran limechukua pia hatua za kujitengeneza makombora ya vita vya angani.

Katika miaka ya hivi karibuni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepata mafanikio makubwa katika sekta yake ya ulinzi ambapo imeweza kujitosheleza katika uzalishaji wa zana na mifumo muhimu ya ulinzi. Februari pili mwaka huu, Iran ilizindua ndege yake mpya kabisa ya kivita ijulikanayo kama Qaher-313 yaani mshindi. Ndege hiyo yenye uwezo wa kukwepa rada ilibuniwa na kutengenezwa kikamilifu na wataalamu wa Iran. Ndege ya kwanza ya kivita kutengenezwa Iran ni ile ijulikanayo kama Azarakhsh. Aidha Iran imetengeneza ndege ya kivita ijulikanayo kwa jina la Saeqeh ambapo squadron yake ya kwanza ilizinduliwa mwaka 2010.

Mara kwa mara Iran imeyahakikishia mataifa mengine kuwa uwezo wake wa kijeshi si tishio kwa nchi zingine bali sera za kijeshi za Jamhuri ya Kiislamu zimejengeka katika msingi wa kujihami.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...