Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na
kuongezeka machafuko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, umoja huo
una wasiwasi kuhusiana na kuongezeka mapigano baina ya jeshi la Congo
DRC na wapigani wa waasi wa M23 huko mashariki mwa nchi hiyo. Farhan Haq
amebainisha kwamba, usalama umevurugika mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo baada ya kuzuka mapigano baina ya jeshi la nchi
hiyo na waasi wa M23. Aidha amesema, Umoja wa Mataifa umeanzisha
uchunguzi kuhusiana na kuuawa waandamanaji wawili mjini Goma, makao
makuu ya jimbo la Kivu Kaskazini, maandamano ambayo yalifanyika kulaani
mauaji dhidi ya raia pamoja na ukosefu wa amani mashariki mwa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment