Monday, August 19, 2013

LEO KATIKA HISTORIA

Leo ni Jumatatu Agosti 19,2013 , Siku kama ya leo miaka 94 iliyopita, yaani tarehe 19 Agosti mwaka 1919, kwa mara nyingine tena nchi ya Afghanistan ilipata uhuru.

 Katika miaka ya nyuma, nchi hiyo aghalabu ilikuwa chini ya uongozi na tawala mbalimbali. Kwa mara ya kwanza uhuru wa Afghanistan ulitangazwa mwaka 1747 na Ahmad Shah Abdali. Hata hivyo takriban karne moja iliyofuata Waingereza wakiwa na lengo la kulilinda koloni lao kubwa la India, walianza kuingilia mambo ya ndani ya Afghanistan na kupelekea kuzuka vita vya kwanza kati ya Uingereza na Afghanistan.

 Uingereza ilipata hasara kubwa katika vita hivyo na kulazimika kurejea nyuma. Hata hivyo Waingereza waliendelea kuingilia mambo ya nchini humo hadi vilipojiri vita vya pili kati ya pande mbili hizo mnamo mwaka 1905. Mwaka 1919 Amanullah Khan alifanikiwa kuwa Gavana Mkuu wa Afghanistan na kufuta mikataba yote baina ya nchi hiyo na Uingereza na kisha akatangaza uhuru wa nchi hiyo. 

 Siku kama ya leo miaka 351 iliyopita, sawa na Agosti 19 mwaka 1662, aliaga dunia Blaise Pascal mwandishi, malenga wa Kifaransa na mgunduzi wa Calculator au kikokotoo. Alizaliwa mwaka 1623 na aliondokea kupenda sana taluma ya hisabati tangu akiwa kijana mdogo. Aidha hatua ya baba yake ya kuwa na marafiki wasomi, ilichangia mno katika kuchanua kipaji ya Pascal.

Na miaka 60 iliyopita siku kama ya leo mwafaka na tarehe 28 Mordad mwaka 1332 Hijria Shamsia, Marekani ilifanya mapinduzi nchini Iran na kuiondoa madarakani serikali ya Dakta Musaddiq na kwa muktadha huo, Muhammad Reza Pahlavi akarejea tena madarakani. Mapinduzi hayo yalipangwa na kuongozwa na Shirika la Ujasusi la Marekani CIA likishikiana na Uingereza.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...