Monday, August 19, 2013

RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA AWASILI CHINA NA KUPATA HESHIMA YA KUPIGIWA MIZINGA 21


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye yuko ziarani nchni China na amepokea heshima ya kupigiwa mizinga 21 na anatarajia kuwa ziara yake itasaidia kuhimiza zaidi uhusiano kati ya Kenya na China.

 Rais Kenyatta amesema Kenya inalenga kuimarisha zaidi ushirikiano na China katika maendeleo ya miundo mbinu pamoja na miradi mingine muhimu.

 Ametaja miradi itakayopewa kipaumbele kuwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa na viwanja vya ndege. Pia amesema China ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa Kenya, na ni wazi kuwa Kenya itajifunza mengi kutokana na ushirikiano huo. Rais Kenyatta aliwasili jana nchini China ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini China tangu achaguliwe kuwa rais wa Kenya.

 Katika ziara hii inayolenga zaidi mambo ya uchumi, rais kenyatta ameambatana na ujumbe mkubwa unaojumuisha mawaziri na wafanyabiashara kadhaa wakubwa wa Kenya.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...