------------------------------ ------------------------------ ------
Na Nathan Mtega wa Demashonews,Songea
MTANDAO wa polisi
wanawake mkoani Ruvuma umeanza maadhimisho ya wiki ya polisi wanawake kwa
kutembelea na kutoa msaada kwa wagonjwa wanawake na watoto katika hospitali ya
rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea.
Akizungumza mwenyekiti wa mtandao huo wa polisi wanawake
Mrakibu msaidizi wa polisi Anna Tembo amesema lengo la kutembelea katika
hospitali hiyo ni kutoa msaada kidogo pole na hongera kwa wagonjwa waliolazwa ambao ni wanawake
waliojifungua watoto chini ya umri wa
miaka mitano pamoja na kuwafariji wagonjwa kwa ujumla.
Amesema pia ni kuifanya jamii itambue kuwa polisi ni sehemu
ya jamii ambayo inapaswa kushirikiana na jamii kwa kila jambo na si kwa masuala
ya kulinzi na usalama wa watu na mali zao pekee na ushirikiano huo unapaswa
kuwepo kwenye idara zote na jamii kwa ujumla.
Amesema kuwa kumekuwepo na matukio mengi ya ukatili kwa
watoto yanayofanywa na wazazi ambao ni wanawake na wanaume hivyo maadhimisho
hayo yatatumika pia kwa kuifanya jamii kujenga upendo miongonimwao na hasa kwa
watoto ambao wamekuwa ndiyo waathirika wakubwa wa matukio hayo ukatili ambao
umekuwa ukifanywa na wazazi wao kwa sababu mbali mbali huku baadhi ya wanawake
wakiwatupa watoto wao baada ya kujifungua kwa kushirikiana na wanaume baada ya
kudanganyana kuhusu kuoana.
Mwenyekiti wa mtandao huo pamoja na kuiasa jamii kuhusu
vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake ambavyo baadhi vimekuwa vimekuwa
vikitokea kwa sababu ya kukosekana kwa upendo kwa wanandoa ameshauri kuutumia
mtandao huo wa polisi ambao unafanya kazi kwa ushirikiano na kituo cha msaada
wa kisheria cha mjini Songea kwa kuwsilisha matatizo yao mbali mbali ili yaweze
kupatiwa ufumbuzi kwa njia ya amani.
Akizungumzia ujio huo wa askari polisi wanawake hospitalini
hapo Afisa muuguzi kiongozi wa hospitali hiyo
Marcella Wella mbali ya kuwashukuru askari polisi hao kwa uamuzi huo
lakini ameiomba jamii kutambua kuwa polisi nao ni sehemu ya jamii na wanaonesha
ushirikiano mkubwa na jamii inapaswa kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.
Amesema kuwa jamii imekuwa na mtazamo hasi kwa askari wa
jeshi la polisi kwa kujengeka na imani kuwa askari polisi wapo kwa ajili ya
ulinzi na usalama wa raia na mali zao tu lakini kitendo cha askari polisi hao
kupitia mtandao wao kufika na kuwafariji wagonjwa wakiwemo wanawake na watoto kwa
kutoa msaada wa vitu mbali mbali zikiwemo sabuni,madishi na nguo ni ishara kuwa
askari polisi nao ni wana jamii ambao wnaonesha ushirikiano mkubwa na jamii
wanayoitumikia hivyo ni wajibu wa kila mmoja kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.
Naye mkuu wa kituo kikuu cha polisi cha mjini Songea mrakibu
msaidizi wa polisi Mashimbi ameitaka
jamii kukitumia kitengo hicho cha mtandao wa polisi wanawake kwa kutoa
malalamiko yao yanayohusiana na unyanyasaji wa aina yoyote kwa sababu vitendo
hivyo vipo kwa kila mmoja na si kwa wanawake pekee.
Amesema kuwa zipo taarifa za wanaume kunyanyaswa na wanawake
lakini wamekuwa wakiona aibu kutoa taarifa za unyanyasaji wanaofanyiwa hali
ambayo hupelekea kujichukulia sheria mkononi na kuleta madhara makubwa kwa
wanafamilia hivyo ni vyema wakautumia mtandao huo wa polisi wanawake kutatua
matatizo yao na kujenga utamaduni wa upendo miongoni mwao.
No comments:
Post a Comment