Friday, August 30, 2013

MWANAJESHI WA TANZANIA AUAWA NA M23 DRC


PICHA YA ASKARI WA TANZANIA WAKIWA KATIKA SHUGHULI ZA UOKOAJI
ASKARI WA TANZANIA WANAOLIOPO KATIKA VIKOSI VYA KULINDA AMANI VYA UMOJA WA MATAIFA DRC
Askari wa Umoja wa Mataifa raia wa Tanzania ameuawa na wengine watano raia wa Afrika Kusini na Tanzania kujeruhiwa katika mapigano na waasi wa M23 huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Msemaji wa vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Kongo Madnodje Mounoubai amesema askari huyo wa kulinda amani ameuawa katika mapigano yaliyojiri Jumatano wakati waasi walipokuwa wakipambana na wanajeshi wa serikali ya Kongo Kinshasa wanaopata himaya ya askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa. Mapigano hayo yalijiri karibu na mji wa Goma ambao ni mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema askari huyo aliuawa baada ya kuangukiwa na maroketi ya waasi wa M23. Jana ngome za waasi wa M23 zilishambuliwa kwa helikopta za jeshi la Umoja wa Mataifa na mizinga ya jeshi la Kongo karibu na mji wa Goma. 

Jeshi la Kongo linapata msaada wa kikosi cha askari 3,000 wa Umoja wa Mataifa ambao wanaidhini maalumu ya kupigana ana kwa ana na makundi ya waasi wenye silaha katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini. Kikosi hicho kinajumuisha wanajeshi wa Tanzania, Malawi na Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...