Saturday, August 10, 2013

SHEIKH PONDA ADAIWA KUPIGWA RISASI MKOANI MOROGORO

KATIBU WA JUMUIYA YA TAASISI ZA KIISLAMU TANZANIA SHEIKH PONDA ISSA PONDA

KAMANDA WA POLISI MKOANI MOROGORO FAUSTINE SHILOGILE
Jeshi la polisi mkoani Morogoro linaendelea kutafuta ukweli kuhusu madai ya kupigwa risasi kwa katibu wa Jumuiya ya Taasisi za kiislam Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda.

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro bw Faustine Shilogile amesema hayo wakati akizungumza moja kwa moja na Radio One kuhusu madai ya kupigwa risasi kwa sheikh huyo.

"Hata sisi tumepata taarifa hizo na ndizo zilivyoenea hapa mkoani Morogoro na tunahangaika huku na kule kuthibitisha kama kweli kapigwa risasi",alisema kamanda Shilogile.

Alipotakiwa kueleza kwa nini kumekuwa na taarifa hizo ambazo wao bado hawana uhakika nazo,amesema Sheikh Ponda kwanza  anatafutwa na jeshi la polisi,na alifika kwenye kongamano la wahadhiri wa mkoa wa Morogoro dakika kumi kabla mkutano haujaisha,na alipewa nafasi ya kuzungumza kwa dakika tano,hivyo mara baada ya mkutano kumalizika wafuasi wake wakawa wanalisukuma gari lake na polisi walikuwa wanataka kumkamata kwa kuwa anatafutwa na jeshi hilo,ndipo wafuasi wake walipomzingira na kumtorosha.

kuhusu nani anaedaiwa kumpiga risasi,kamanda Shilogile anasema wananchi wanadai polisi ndiyo wamefanya hivyo madai ambayo amesema anayafanyia kazi lakini walipojaribu kufika katika hospitali ya mkoa wa Morogoro ambako inadaiwa alifikishwa hakukuwa na taarifa zozote za kufikishwa hospitalini hapo na polisi wanazunguka katika hospitali mbali mbali kutafuta kama amefikishwa huko.
Endelea kufuatilia blog hii kwa taarifa zaidi kuhusu tukio hili.

1 comment:

  1. Si ajabu siku hizi watu kupigwa risasi hapa Tanzania matukio hayo yamekuwa mengi sawa na ukisikia Mwaipaya ana Malaria!

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...