.
WAZIRI MKUU WA THAILAND BI YINGLUCK SHINAWATRA AKISALIMIANA NA VIONGOZI MBALIMBALI |
Serikali
ya Tanzania kupitia wizara ya maliasili na utalii imetiliana saini
mkataba wa miaka mitatu wa ushirikiano katika uhifadhi wa mali asili na
utalii na serikali ya Thailand ikiongozwa na waziri mkuu wake Mh.
Yingluck Shinawatra.
Makubaliano hayo yamesasainiwa na waziri wa mali
asili na utalii wa Tanzania kwa kumuhusisha naibu waziri mkuu wa
Thailand Plodprasop Suraswad, mbele ya waziri mkuu huyo wa Thailand
kwa kuelezwa kuwa ni mwanzo mzuri katika kukuza sekta ya utalii nchini
na kuchangia ukuaji wa uchumi. Akizungumza baada ya kutiliana saini
katika mkataba huo,waziri wa mali asili na utalii Mh. Balozi Khamis
Kagasheki, amesema mbali na kukuza uchumi na utalii wa Tanzania, lakini
pia makubaliano hayo yatasaidia kukuza kipato cha mtanzania kwani sekta
ya utalii inachangia kwa asilimia 17 katika pato la taifa..
Kwa upande wake waziri wa uwekezaji na uwezeshaji
nchini Mh Mary Nagu,amesema ujio wa waziri mkuu huyo wa Thailand hapa
nchini kutawapa fursa wawekezaji wa Thailand kuja kuwekeza nchini
katika sekta mbalimbali.
Ziara hii ya siku moja ya waziri mkuu wa Thailand
katika hifadhi ya taifa ya Serengeti ambao ni miongoni mwa maajabu saba
ya Afrika,imepokelewa kwa furaha kubwa na viongozi wa mkoa wa Mara na
wadau wa sekta ya utalii mkoani Mara.
No comments:
Post a Comment