Usain
Bolt tena akizongwa na waandishi wa habari baada ya kushinda medali
yake ya pili ya michuano ya dunai ya riadha huko Moscow.
Usain
Bolt ametisha tena duniani kwa kunyakuwa taji la 13 la dunia kwa
ushindi wa mbio za mita 200 katika michuano ya dunia ya mbio mjini
Moscow.
Bolt raia wa Jamaican ameshinda mbio hizo kwa kutumia muda wa sekunde
19.66 ikiwa ni siku sita baada ya kutwaa mbio za mita 100.
Mpinzani
wake ambaye ni rafiki yake wa mazoezi Warren Weir ameshinda medali ya
fedha kwa kushika nafasi ya pili akitumia muda wa sekunde 19.79 huku
Mmarekani Curtis Mitchell akishinda medali ya shaba baada ya kutumia
sekunde 20.04.
Adam
Gemili, ambaye katika nusu fainali siku ya Ijumaa alikuwa mwingereza
pekee kuvuka muda wa sekunde 20 alipokimbia kwa kutumia sekunde 19.98,
hakuweza kufanya hivyo hii leo lakini ameshika nafasi ya tano kwa
kutumia sekunde 20.08.
Baada ya kufanikiwa kushinda mbio za leo, alionekana akishangilia pamoja na Weir wimbo wa Bob Marley wa 'Three Little Birds'.
No comments:
Post a Comment